June 29, 2019


Baada ya iliyopita Jumatano kusambaa taarifa zinazomuhusu kiungo wa Simba, James Kotei kutimkia katika Klabu ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini, aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema Simba wamefanya makosa kumuachia mchezaji huyo.

Kotei aliyejiunga na Simba Disemba 2016 ametwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA mara moja huku akiisaidia Simba kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Julio amesema kitendo cha Simba kumuacha mchezaji huyo ni kosa kubwa ambalo watalijutia kwa muda mrefu kwa kuwa kiungo huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji wanaofanya kazi kwa ufasaha akiwa dimbani.

"Simba wamekosea sana kumuacha Kotei, sielewi maamuzi hayo kayafanya nani.
"Hauwezi kumuacha mchezaji kama Kotei ambaye kila mmoja alikuwa anajua kazi yake akiwa uwanjani.

"Mimi naamini pengo la Kotei litawaumiza na watakuja kujutia uamuzi wao, hauwezi kumuacha mtu ambaye ameshaifahamu Simba na kutegemea watu ambao hauna uhakika kama watapafomu, sijui pale Simba kuna kitu gani," amesema Julio.

5 COMMENTS:

  1. Sasa yeye ndie kocha wa Simba?Kwanini sisi wabongo wabongo huwa wazuri wa maneno tu?Yeye jamhuri hata kumanage timu ya daraja la kwanza kunamshinda.

    ReplyDelete
  2. Kotei hatujamuacha kachagua maisha kwingine kama samatta alivyohitajika mazembe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio kweliii simba hawakuwa na mpngo na Kotei ktk msimu ujao kwani alikuwa unasubiria kuongezewa ila ndio hvyo Lengo la Kotei lazima lionekane msimu ujao hakuna namna

      Delete
  3. Huo ndio ukweli. Kotei bonge la mchezaji. Ni kama vile umuache Tshabalala nadir wachezaji wa uhakika. Sio kitu naamini yupo atakayeliziba pengo

    ReplyDelete
  4. Huu mwaka hawana Chao,tulia uone.kocha Uchebe atafukuzwa asubuhi tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic