June 28, 2019


WACHEZAJI wapya wa Yanga na wale wa zamani wanatarajia kuanza kuingia nchini wiki hii kwa ajili ya kujiandaa na kambi ya timu hiyo inayotarajiwa kuanza rasmi Julai 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Tayari Yanga imeshasajili nyota 10 wapya wakiwemo wazawa ambao ni Mapinduzi Balama, Abdulaziz Makame,Ally Ally, kwa upande wa wageni ni Patrick Sibomana, Sadney Urikhob, Issa Bigirimana ‘Wacott’, Maybin Kalengo, Juma Balinya, Lamine Moro na Suleiman Mustapha.

Mratibu wa kikosi hicho Hafidh Saleh alisema, wanatarajia kuingia kambini Julai 7 mwaka huu hivyo kwa kuwa hawatakuwa na muda wa kuchelewesha ‘programu’ wachezaji wale waliopo nje ya nchi wanatakiwa kuanza kuingia kwenye Uwanja wa Ndege nchini kuanzia mwishoni mwa wiki hii.

“Tunatarajia kuanza maandalizi mapema maana mbele yetu tutakuwa na mchezo wa kirafiki siku ya kilele cha tamasha letu la Mwananchi, ambapo pia siku hiyo itatumika kuwatambulisha nyota wapya na kikosi chote kwa ujumla kama ilivyotangazwa hivi karibuni pale Diamond Jubilee.

“Sina taarifa rasmi kama kambi itakua nchi gani zaidi nafahamu maandalizi ya awali yatafanyikia hapahapa kwa zaidi ya wiki mbili nadhani baada ya hapo kocha ndiyo atatoa muongozo wake na mahali gani tutahamishia kambi mapema kabla ya msimu mpya kuanza,” alisema Hafidh.

2 COMMENTS:

  1. Kazi ipo Simba ubingwa muusahau, huo ni usajili WA Kalamu na mstari juu ya paper nyeupe

    ReplyDelete
  2. Mtacheza na sisi mechi mbili kati ya 38. Hata hizo mbili mtatuachia pointi 6 zote. Kama hauamini tunza hii comment kisha uje upost baada ya mechi zote mbili.
    Kocha wenu kawachanganya wenzake akidhani ni yeboyebo wale, wamepoteza game mbili kati ya tatu afu anatoa sababu mlenda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic