June 29, 2019


BAADA ya James Kotei kusepa mazima Simba na kutimkia kikosi cha Kaizer Chief ya Afrika Kusini kwa kandarasi ya miaka mitatu mambo yamezidi kupamba moto Simba.

Mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Deogratius Munish 'Dida' ametoa mkono wa kwa heri kwa mashabiki wa Simba.

Dida alisajiliwa na Simba kwa kandarasi ya mwaka mmoja tayari mkataba wake umemalizika na sasa ni mchezaji huru ambaye amesema anahitaji kupata changamoto mpya.

"Napenda kuwashukuru mashabiki zangu, uongozi wa Simba kwa muda ambao nimewatumikia, kwa sasa nahitaji kupata changamoto mpya," amesema Dida.

Dida anakuwa mchezaji wa nne kuaga Simba akiungana na kiungo mnyumbulifu, Haruna Niyonzima ambaye naye amesema kuwa muda ukifika atataja sehemu atakayokuwa msimu ujao, pamoja na mshambuliaji Emmanuel Okwi ambaye amesema ni ngumu kusema neno kwa heri.

4 COMMENTS:

  1. NAMUNGO FC inawuhusu....

    ReplyDelete
  2. Bila yakuwa mwanaume wa mpambanaji mgumu pale simba lazima utakimbia au utakimbizwa.Wanasema kwenye vita ndipo kwenye fursa kubwa zaidi ya kiuchumi na Shujaa pekee ndie panamuhusu.

    ReplyDelete
  3. Sijui wachezaji wa Simba wamenogewa na hela za mo,au sababu ni nini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic