STARS YAENDELEA KUKALIA MKIA KUNDI C AFCON, YACHAPWA 3-2 NA KENYA
Kikosi cha Taifa Stars kimpoteza tena mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika awamu hii dhidi ya Kenya kwa kuchapwa mabao 3-2.
Kipigo hiki kimekuwa cha pili baada ya mechi ya kwanza kufungwa mabao 2-0 na Senegal.
Mabao ya Kenya yamefungwa na Michael Olunga aliyeingia kambani mara mbili huku moja likiwekwa kambani na Johanna Omolo.
Wakati Stars imefunga mabao yake kupitia kwa Mbwana Samatta na Simon Msuva.
Stars sasa itakabiliwa na kibarua kingine dhidi ya Algeria Jumatatu kunako kundi C ambapo mpaka sasa haina alama hata moja.
Unajua hakuna Mtanzania anaeichukia Taifa stars kutotaka kuona inapata mafanikio.Taifa stars ni moja ya mabalozi wetu muhimu sana kwa nchi yetu. Na kila ukiona mtanzania anaikosoa sana timu hiyo basi ujue ni mzalendo zaidi na anaipenda zaidi timu hiyo na wala sie adui wa nchi au mamlaka.Najua kuna watu wanapoona TFF au Taifa stars inakosolewa basi huegemea zaidi kunako siasa ila hata TFF kwa kutumia mgongo wa siasa basi wamepata kichaka cha kujifichia madhaifu yao. Tunaposema TFF wamekosea katika suala la uteuzi wa kocha wa Taifa stars sio kwamba wanaonewa bali makocha wana viwango vyao na sio suala la kubahatisha ni open and clear ni kama vile vitu vivyokwisha tengenezwa tayari vipo sokoni vinavyotofautiana ubora. Na ni maamuzi ya mnunuzi nini anataka.
ReplyDeleteTulipofungwa na Senegali tukafurahi kwakuwa hatukufungwa goli nyingi. Kwa kweli wakati mwengine Watanzania lazima tujitafakari kwani ni jambo la kushangaza kuona tunafurahia kufungwa. Tuna fungwa na senegali tunafanya sherehe vipi tukifungwa magoli kidogo na wajerumani? Nadhani tunaweza hata kuwagia vipande vya mbuga za wanyama wachezaji wa Taifa stars. Kumbe senegali ni timu ya kawaida tu sio malaika na wanafungika? Taifa stars ilipofungwa na Senegali tukaona kama tumefungwa na malaika yaani ni wambinguni kabisa na kwa kila mtu alie na mawazo mbadala yakwamba kweli Senegal wazuri ila Taifa stars ni ya hovyo hasa kwenye eneo la kocha na benchi lake la ufundi basi mtu mwenye maoni kama hayo alionekana adui. Ila hata hili la kufungwa na Kenya basi kwa jinsi tunavyojifahamau sisi watanzania kwa kuwa tumeshajikubalisha na unyonge basi huu ni ushindi mkubwa sana kwetu sisi yaani kufungwa goli 3-2 kwetu sisi ni ushindi tena mkubwa sana sasa kama si ujinga kitu gani? Amunike amekuja kuivuruga zaidi Stars na sijui kwa malengo gani nadhani ni katika ile hali ya kujifundisha kazi ila watanzania bado tumelala sana na tutaendelea kulala na tutalazwa sana na mataifa mengine. Na kama invyojulikana hata sudani kusini wamekuja na watatutangulia muda si mrefu kunako michezo na kutuwacha tunaendelea kulala. Amunike amekuja kutugawa watanzania. Taifa stars ilipaswa kuongozwa na kocha mwenye busara ziadi ila na nadhani wadau kwakuwa wanakereka pale watu wanaposema ukweli kwa taifa stars basi naona kitakachofuata kwa watanzania wapenda michezo hasa mpira wa miguu ni kupuuza timu hiyo ya Taifa stars. Binafsi sita koment au kusema tena kitu chochote kile kuhusiana na taifa stars kwani is just like wasting of time for nothing.
Ni kocha gani kwenye busara amewahi fundisha stars!? Kufungwa ni sehemu ya mchezo, hao kwenye busara mbona hatukwenda afcon kwa zaidi ya miaka 39? Tuliqualify michuani ya wachezaji wa ndani, tulifanya nini zaidi ya kufungwa!? Unaweza kutofautisha Senegal na Ujerumani!? Hivi unajua kikosi kilichomfunga ufaransa tena akiwa bingwa wa dunia hakikuw na ubora kama Senegal ya sasa!? Amunike sio malaika lakini lazima tukubali pia amefanya kazi yake.Acheni tujifunze, tukirudi tena tutakuwa tumekomaa!!
DeleteKocha Hatuna Na Hata Afcon Kushiriki Ni Huruma Za Uganda Pamoja Caf Kuongeza Timu Lakini Aumunike Haja Tupeleka Afcon So Huyo Hafai Kuifundisha Stars
DeleteHatuna kocha hapo.Unaposhiriki mashindano kama ya Afcon ina maana unakwenda kushindana na sio kujifunza au kufanya majaribio ya wachezaji na mifumo.Siwalaumu TFF bali wanasiasa ndio tatizo ktk soka letu la bongo na huo ndio ukweli wenyewe.
DeleteInashangaza sana kusikia watu wenye akili zao wakitamka bila ya aibu eti Amunike ametupeleka Afcon baada ya miaka 39? Hapo ndipo unapojua yakuwa watanzania ni bure kabisa vichwani mwetu. Taifa stars imeingia Afcon kwa kusua sua na ni ukweli usiopingika yakwamba katika mechi ya mwisho ya makundi yakufuzu Afcon kati ya Uganada na Tanzania ilikuwa ni ya bonanza kwa Uganda.walikuwa hawana cha kupoteza kwani waganda walikuwa walishafuzu tayari.Yaani kiukweli kabisa Uganda waliamua kuibeba Tanzania kwenda Afcon hakuna ubishi na kama tungekuwa watanzania tunajitambua zaidi basi Amunike alikuwa atimuliwe kazi baada ya mechi ya Lethoso nadhani hata yeye mwenyewe alikuwa akitarajia hivyo ila ndio hivyo tena akakutana na watu wasiojua nini wanafanya wapo wapo tu.
ReplyDeleteHapa hatuna kocha bwana,hii michezo tunafungwa yote,kuna watu sijui wanatetea upuuzi gani?team inajiendea bila direction,hakuna kinachovutia kwa stars,butua butua tu.
ReplyDeleteNakubaliana na wewe Brother kazi kubwa ni butua butua.Baada ya robo saa nilikuwa na uhakika wa kupokea kichapo.Wakenya wanacheza mpira wa kutulia sisi kelele nyingi na piga piga ovyo.
Delete