June 29, 2019




Na Saleh Ally, Cairo
Hivi ndio vikosi vitatu vya Senegal, Algeria na Kenya vilivyo katika kundi moja katika michuano ya Afcon na timu yetu ya Tanzania.

Unaweza kuangalia na kuona kikosi kipi kina wachezaji bora zaidi na kwa nini?

Katika maoni, kuwa huru kupanga kikosi cha kwanza hadi cha nne kwa maana ya kile ulichoona ni bora zaidi.


Kikosi cha Senegal vs Algeria
Edouard Mendy (Stade De Reims)
Kalidou Koulibaly (Napoli)
Cheikhou Kouyate (Crystal Palace)
Mbaye Niang (Stade Rennais)
Sadio Mane (Liverpool)
Keita Balde (Inter Milan)
Youssouf Sabaly (Bourdeux)
Alfred Ndiaye (Malaga)
Krepin Diatta (Club Bruges)
Papa Ndiaye (Galatasaray)
Moussa Wague (Barcelona)

Kikosi cha Algeria vs Senegal
Adi-Rais Cobos Mbolhi (Ettifaq)
Aissa Mandi (Real Betis)
Djamel Eddine Benlamri (Al Shabab)
Riyad Mahrez (Manchester City)
Mohammed Youcef Belaili (Esperance)
Baghdad Bounedjah (Al Sadd)
Sofiane Feghouli (Galatasaray)
Adlane Guedioura (Nottingham Forest)
Youcef Atal (Nice)
Amir Rami (Stade Rennais) 
Ismael Bennacer (Empoli)


Kikosi cha Tanzania vs Kenya
Aishi Manula (Simba)
Gadiel Michael (Yanga)
Erasto Nyoni (Simba)
Kelvin Yondani (Yanga)
David Mwantika (Azam)
Mbwana Samatta (Genk)
Thomas Ulimwengu (JS Saoura)
Simon Msuva (Diffa El Jadida)
Farid Mussa (Tenerife)
Hassan Kessy (Nkana FC)
Mudathir Yahya (Azam)


Kikosi cha Kenya vs Tanzania
Matasi Patrick (St. George)
Joseph Okumu (Real Monarchs)
Abud Omar (Sepsi OSK)
Mohamed Musa (Nkana FC)
Masika Ayub (Beijing Renhe)
Johana Omolo (Cercle Bruges)
Francis Kahata (Gor Mahia)
Victor Wanyama (Tottenham)
Erick Otieno (Vasalund)
Michael Olunga (Kashiwa Reyson)
David Owino (Zesco United)

4 COMMENTS:

  1. 1: Senegal 2: Algeria 3: Kenya 4: Tanzania.

    Maoni yangu ni kwa kuzingatia uwezo wa mchezaji mmoja-mmoja na ubora wa ligi na klabu wanazochezea.

    ReplyDelete
  2. Kabla ya AFCON hakuna asiejua kuwa Tanzania hatuna wachezaji wanaocheza nje ya nchi kulinganisha na washiriki wengine wa Afcon sasa cha ajabu kitu gani?
    Katika maisha kila kitu ni fursa kwa watu wenye vichwa vyenye kufanya kazi sawa sawa. Kutokana na madhaifu yetu kama watanzania basi tunaweza kuwa na wachezaji wote wa Taifa stars wakawa wanacheza nje ya nchi kwenye klabu kubwa tu duniani na matokeo yake tukawa na ushiriki wa hovyo wa Afcon kuliko hata hii stars ya sasa. Angetafutwa tu Kocha mmoja mpumbavu kutokana na mahusiano yake na viongozi wa Taifa stars hata kama uwezo ni mdogo halafu akakabidhiwa timu ya Taifa kwisha habari.Brazili wakati wanapigwa saba 7-0 na wajerumani kwenye kombe la Dunia walikuwa na zaidi ya wachezaji mia nane 800 wanaocheza vilabu vinavyojulikana Europe yaani ulaya peke yake. Kinachosikitisha kwa Taifa stars na wadau wanashindwa kufahamu au wanafahamu ila wanaranguliza siasa mbele ni kwamba tumepoteza fursa moja muhimu na adimu sana kwenye umri wa Tanzania kwenye mashindano haya ya AFCON.Ishu hapa sio tuna wachezaji wangapi wanaocheza nje ya nchi bali ishu muhimu ni tulijiandaa vipi kuikabili Afcon baada ya miaka arubaini bila ya kushirki? Je malengo makubwa yalikuwa ni nini hasa kwenye ushiriki wetu wa Afcon hii? Na Kama kweli watanzania tunaamini kuwa tatizo la Taifa stars ni kukosa wachezaji wa kutosha wanaocheza nje kwenye nchi zenye uwezo zaidi hasa ulaya,je tuliweka mikakati gani kuhakikisha tunakwenda kuuza wachezaji wa kutosha kupitia Afcon? Yaani sie lengo letu kwa Afcon lingekuwa moja tu kwenda kuzishawishi klabu bora zaidi duniani kuvutiwa na wachezaji wetu. Yaani tungepigana piga Uwa kuwaandaa wachezaji wa Taifa stars kwa makusudi maalum kwa ajili ya kwenda kuonekana duniani wakiwa katika ubora wao hata kama wangepoteza mchi,je wahusika walifikiria hivyo na walitumia hilo?Siku zote watu wanasema Tanzania kuna vipaji vya mpira na amini usiamini siku Taifa stars inacheza na Senegeli wapenda mpira wengi duniani nadhani hata mawakala waliacha shughuli zao kwa ajili ya kuiangalia Tanzania ili kuona kitu kipya .Siku zote binaadamu huwa na shauku na kitu kipya na Tanzania ni mpya kwenye Afcon. Ni sawa na mgodi wa dhahabu uliokuwa hauaja chezewa bado watu wakiwa na shauku ya kuvuna madini lakini la kusikitisha kilichoonekana kwa taifa stars kiliwavunja moyo watu wengi sana. Kwani kutokana na kazi au mfumo wa kocha wao Taifa stars imeonekana ni timu isiostahili hata kuwemo kwenye fainali hizo muhimu na kubwa kuliko mashindano yote barani Africa. Tatizo ni moja tu kwa Taifa stars nalo ni maadalizi ya hovyo kwa timu hiyo hasa kwa wahusika kutokuwa makini katika uteuzi wa makocha bora wa kuwafunda vijana kulingana na matarajio yetu na ukubwa wa mashindano husika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic