June 22, 2019


Kiungo Mapinduzi Balama amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na klabu ya Yanga.

Kiungo huyo amefikia makuabliano na Yanga  akitokea Alliance FC ya Mwanza.


Usajili huo unaendelea ikiwa ni moja ya maboresho yanayofanywa na uongozi wa klabu ili kujiandaa kuelekea msimu ujao.

Ikumbukwe kwa Mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Fredrick Mwakalebela, alisema kuwa wanafanyia kazi ripoti ya Kocha Mkuu Mwinyi Zahera ambaye yuko Misri.

Zahera yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Congo akiwa kama Kocha Msaizidi.

4 COMMENTS:

  1. Hata Piusi Baswita wa mbao ulikuwa ni usajili wa kutisha.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakwambia vijana wadogo wanapotea...hata sijui Pius Buswita atapata mkataba mpya?...Kwa nini vijana wetu wengi hawajitambui wakiangalia mifano ya kina Eliud Ambokile aliyesajiliwa TP Mazembe au Kiyombo alienda Mamelodi Sundowns?wametokea Simba au Yanga?Nafikiri tatizo liko kwa mawakala wanaofaidika kwa migongo ya wachezaji.Angalia Salamba....Pius Buswita....Pato Ngonyani....Moses Kitandu...Bora Nkomola alijistukia

      Delete
    2. Issue ni kutojitambua, mbona wanaotoka nje wanatusua!! Mbona wapo waliopita Yanga na Simba na wakatusua!! Kuna watu wanalea vijana kama Azam!? Mbona vijana wengi wamepotea

      Delete
  2. Tatizo lililopo ktk timu zetu hakuna wataalamu wa psychology na ya mpira hasa kwa vijana wadogo wanaosajiliwa timu kubwa.
    Pesa za usajili huwa zinawachanganya saaana,la laiti kama wangepata watu sahii wa kuwaelimisha,wasingepoteza vipaji vyao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic