July 12, 2019



 AS Vita ya Congo imethibitisha kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Yanga siku ya Agosti 4 mwaka huu uwanja wa Taifa kilele cha siku ya Wananchi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa timu ya AS Vita imekubali kuja Bongo kucheza mchezo huo wa wa kirafiki.

“Tumecheza na timu nyingi kubwa na tumepata matokeo chanya hivyo hatuna mashaka na kikosi chetu kuelekea kwenye mchezo wetu wa kilele cha Wananchi dhidi ya AS Vita uwanja wa Taifa.

“Timu itawasili Bongo, Agosti 2 na itafanya mazoezi Agosti 3 kisha itakuwa kazini Agosti 4 mashabiki wajitokeza kwa wingi kushuhudia namna kikosi kitakavyopambana," amesema Mwakalebela.

12 COMMENTS:

  1. Safi sana yanga.....!!! Hakika tutafika

    ReplyDelete
  2. Safi sana yanga.....!!! Hakika tutafika

    ReplyDelete
  3. unapokipima kkos chako lazma uite tmu kubwa zenye ushndan na ndo unaijua tmu yako sio kama simba day wanavoita tmu ambazo wana uhakka watazfunga mara leopad rayon asante kotoko tmu imeshapotea ndo wanaiita hongeren yanga.

    ReplyDelete
  4. Zahera bwana,! Amemuita rafiki yake amtunzie heshima na ugali!!!

    ReplyDelete
  5. ngojeni mleza uso muanze visingizio

    ReplyDelete
  6. As vita wameamua kuja kulipa fadhila ya jitihada za kufa mtu za Yanga ili waifunge Simba ila mnyama akiwa kwenye himaya yake hata faru akija ataliwa tu .

    ReplyDelete
  7. IYO SIKU YENU YA WANANCHI MJUE TU KUA SIMBA HATUMO

    ReplyDelete
  8. Kwani timu hiyo si ilikuwa mboga tu Kwa Mnyama?

    ReplyDelete
  9. Vita walikufa taifa mbele ya simba hawana jipya

    ReplyDelete
  10. Jipya wanalo ndo maana walikugunga 4 kwao we ukamfunga 2 tena kwa goli LA babu

    ReplyDelete
  11. yanga wanataka kutebelea nyota ya simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic