Abdulhalim
Humud aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu ya KMC kwa sasa yupo kwenye
mchakato wa mwisho kukamilisha dili yake kutimkia Uarabuni kwa ajili ya kupiga
soka la kulipwa.
Habari
kutoka kwa mtu wa karibu zimeeleza kuwa Humud anakamilisha taratibu za
mwisho kutimkia kwenye Falme za Kiarabu kwenda kusakakata soka.
“Mpango wake
mkubwa kwa sasa ni kuondoka Bongo kutokana na mikasa ambayo amekuwa akipitia
ili kujiweka mbali, ila ameshapata timu moja iliyopo kwenye Falme za Kiarabu,"kilieleza chanzo.
Humud
amesema kuwa mipango ya kuondoka ama kubaki itakuwa wazi endapo
mipango itakamilika kwani kwa sasa anakamilisha taratibu za mwisho.








0 COMMENTS:
Post a Comment