July 11, 2019


Aliyekuwa Kiungo wa klabu ya Simba SC, Haruna Niyonzima amekamilisha usajili wake kwa kusaini mkataba wa kuwatumikia mabingwa wa Rwanda Cup, AS Kigali inayoshiriki ligi Kuu Nchini kwao Rwanda.

Niyonzima 29" kaitumikia Simba SC kwa miaka miwili akitwaa ybingwa wa Ligi Kuu Bara misimu yote akiyokaa klabuni hapo.

Kabla ya kutua Msimbazi, fundi huyo aliletwa nchini Tanzania mwaka 2011 na klabu ya Yanga ambayo aliitumikia kwa kipindi cha muda wa miaka takribani mitano na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa misimu minne akiwa na mabingwa hao wa kihistoria.

Baada ya mkataba wake kumalizika Msimbazi, fundi anajiunga na Klabu ya AS Kigali ambao ni wawakilishi wa Rwanda katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika..

Niyonzima ametua nchini kwao Rwanda ambako ana historia ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Rwanda 🇷🇼 Mara tatu.

Niyonzima  pia anaondoka nchini akiwa na historia ya kuwa mchezaji pekee kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tano mfululizo akiwa miamba wawili wa soka ambao ni Simba na Yanga.

2 COMMENTS:

  1. CV nzuri sana, kila la heri fundi, huenda ukatakiwa tena Bongo

    ReplyDelete
  2. niyonzima ameondoka kutokana na kutokuwa kwenye mipango ya kocha au ana sababu zake binafsi???

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic