August 12, 2019


BAADA ya Azam FC kukubali kupoteza mbele ya Fasil Kenema kwenye mchezo wa kwanza wa michuano ya Kombe la Shirikisho sasa kazi imeanza kuelekea mchezo wa marudio.


Azam FC iliyo chini ya Kocha Ettiene Ndayiragije imefungwa bao 1-0 ugenini hivyo ina kazi ya kupindua meza kibabe uwanja wa nyumbani.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Azam Complex.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema dakika 90 za mwanzo zimekamilika kwa kupoteza hivyo hesabu zao ni kujipanga kupata matokeo chanya mchezo wa nyumbani.

"Dakika 90 za awali ugenini tumemaliza kwa kufungwa bao 1-0 sasa mipango yetu ni kwenye mchezo wa marudio nasi tutatumia vema uwanja wa nyumbani ili kusonga mbele," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic