AZAM FC leo wameanza kwa kuchechemea kwenye mchezo wa awali dhidi ya Fasil
Kenema baada ya kukubali kufuungwa bao 1-0.
Mchezo huu wa awali wa Kombe la Shirikisho Afrika umechezwa uwanja wa Bahir, Dar, nchini Ethiopia na bao la ushindi lilipatikana kipindi cha kwanza dakika ya 45
kupitia kwa Bezabeth Meleyo.
Jitihada za
wachezaji wa Azam FC kupata bao la kusawazisha kipindi cha pili ziligonga
mwamba na kufanya mpaka dakika 90 kukamilika wakiwa nyuma kwa bao 1.
Mchezo wa
marudio utachezwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Chamanzi na Azam ina kazi ya
kupindua meza kibabe ili kusonga mbele.
0 COMMENTS:
Post a Comment