Baada ya kikosi cha Azam FC kuitoa Fasil Kenema kwa jumla ya mabao 3-2, sasa kimeanza kujiweka sawa kwa ajili ya kucheza na Triangle United ya Zimbabwe kwenye raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Triangle imefuzu raundi ya kwanza baada ya kuichapa Rukinzo ya Burundi kwa jumla ya mabao 5-0, ikishinda nyumbani 5-0 na ugenini kulazimisha sare ya bila kufungana.
Azam FC itaanzia nyumbani katika mechi ya kwanza itakayopigwa kati ya Septemba 13 na 15 huku ya marudio ikitarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 27 na 29 mwaka huu.
Ettiene Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani kimataifa wanahitaji sapoti ya mashabiki ili kupeperusha Bendera ya Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment