Taarifa zilizopo zinasema kuwa Niyonzima aligomea kusaini mkataba na wekundu hao wa Msimbazi sababu ya kushindwa kufikiana makubaliano.
Makubaliano hayo inaelezwa kuwa Niyonzima alitaka kusainishwa mkataba wa miezi sita pekee kutokana na dau ambalo Simba waliliweka mezani lakini mabosi wake walitaka asaini miaka miwili.
Kutokana na suala hilo, Niyonzima ilimbidi akatae na badala yake akaamua kurejea kwao Rwanda na sasa tayari ameshaanza kazi na AS Kigali.
Kiungo huyo aliyewavutia Simba haswa kuelekea mwisho wa mkataba wake alikuwa nchini hapa siku chache zilizopita alipokuja na AS Kigali kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya KMC.
0 COMMENTS:
Post a Comment