BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 'Tanzanite' amesema kuwa kikubwa kilichowapa ushindi ni kujiamini na kucheza kwa kushambulia.
Tanzanite jana imetwaa ubingwa wa michuano ya COSAFA nchini Afrika Kusini baada ya kuifunga Zambia kwenye mchezo wa fainali mabao 2-1.
Akizungumza na Saleh Jembe, Shime amesema kuwa walipambana kiasi cha kutosha kwa bidii kubwa jambo lililowapa mafanikio.
"Tulikuwa na kazi moja kutafuta matokeo na kulipa kisasi kwa wapinzani wetu kwa kuwa tuliingia uwanjani na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-1 mchezo wa hatua ya makundi.
"Wachezaji wameonyesha juhudi na mbinu kubwa ilikuwa ni kushambulia mwanzo mwisho jambo ambalo limesaidia timu kutwaa ubingwa, shukrani kwa mashabiki kwa sapoti kubwa," amesema.
Michuano hii Tanzanite alialikwa na wenyeji walikuwa ni Afrika Kusini walitolewa na Tanzanite kwenye hatua ya nusu fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment