UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwenye mchezo wa marudio wa kimataifa dhidi ya UD Songo, unaotarajiwa kuchezwa uwanja wa Taifa itakuwa ngumu kwa wapinzani wao kutoka salama kwani wamejipanga kufunga hesabu jumlajumla.
Simba itarudiana na UD Songo ya Msumbiji kati ya Agosti 23-25 ikiwa ni mchezo wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwenye mchezo wa kwanza ambao ulichezwa uwanja wa Beira, Simba ililazimisha sare ya kutofungana hivyo ili kusonga mbele wana kazi ya kushinda kwenye mchezo huo.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa haikuwa kazi nyepesi kwa kikos kufika hapo ila watatumia nafasi ya kuwa nyumabni kushinda.
"Haikuwa malengo yetu kushindwa kupata matokeo ila kwa hatua ambayo tumefikia tuna nafasi ya kushinda tukiwa nyumbani hivyo muda ni wetu wa kufanya yetu kimaaifa.
"Mashabiki wa Simba tujiandae na kazi hii kubwa kwa ajili ya Taifa, kikubwa ni sapoti na imani yetu ni kwamba hatatoka mtu salama pale Taifa," amesema.
2-0 zinatosha
ReplyDeleteitawatosha dozi hii, dozage ya Namna hii Ni ya wastani.
ReplyDelete