BAADA ya
kutolewa rasmi kwenye michuano ya kimataifa uwanja wa Taifa kikosi cha Simba na
UD do Songo sasa wameamua kuitangazia vita mpya Azam FC upande wa makombe ya
kutwaa.
Azam FC
inashikilia makombe mawili kwa sasa ikiwa ni lile la FA na kombe la Mapinduzi,
msimu ujao ina kazi ya kuyatetea baada ya Simba kuyatolea macho yote kwa sasa.
Patrick
Aussems, Kocha Mkuu wa Simba alisema kuwa haikuwa mipago yao kuondolewa michuano
ya kimataifa na timu ya UD do Songo hivyo akili zao zinaelekea kwenye kutwaa
makombe yote watakayoshiriki.
“Tumetolewa
kwenye michuano ya kimataifa ni maumivu makubwa, hivyo tiba yetu ipo kwenye
kutwaa makombe yote ambayo tutashiriki kuanzia sasa kwa kuanza na la ligi
ambalo lipo mkononi.
“Mbali na
kombe la ligi pia tunahitaji kutwaa kombe la FA hata Mapinduzi tukishiriki
lazima tupambane kulitwaa wakati tunajipanga kwa ajili ya msimu ujao kurejea
kimataifa,” amesema.
Kauli hiyo
ni sawa na kutangaza vita kwa Azam FC ambao mipango yao ni kutetea makombe yao
yote mawili waliyonayo mkononi.
0 COMMENTS:
Post a Comment