KOCHA Mkuu
wa timu ya JKT Tanzania, Mohamed Abdallah ‘Bares’ amesema kuwa wanatambua
mchezo wao dhidi ya Simba utakaochezwa kesho uwanja wa Uhuru utakuwa mgumu ila
hawana hofu kwa kuwa wamejipanga kuvuruga hesabu za Simba.
Mchezo huo
ambao ulipangwa kuchezwa Agosti 23 ulipelekwa mbele kutokana na Simba kucheza
michezo ya Ligi ya Mabingwa na wamefungashiwa virago na UD do Songo kwa faida
ya bao la ugenini, uwanja wa Taifa.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Bares amesema kuwa maandalizi yao yapo sawa na
wanatambua Simba ina hasira ya kufungashiwa virago kimataifa wao wamejipanga
kuzivuruga tena.
“Program
yangu maalumu kwa wachezaji imekamilika na wanatambua aina ya timu wanayokwenda
kukutana nayo inataka kuanza kupunguza hasira kwetu hilo litakuwa gumu
kufanikiwa lazima tuvuruge hesabu zao kwanza.
“Mchezo wa
ufunguzi siku zote unatoa picha kamili ya kule unakokwenda sasa wachezaji nao
wanalitambua lazima tufanye kweli, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona burudani
na mpaka sasa hakuna majeruhi,” amesema Bares.
Mchezo wao
wa mwisho uwanja wa Uhuru msimu uliopita JKT alipoteza kwa kufungwa bao 1-0 lilifungwa dakika za usiku na Hassan Dilunga.
Simba atashinda kwa mabao ya kutosha
ReplyDelete