MCHEZO wa Ufunguzi wa Ligi Kuu Bara kati ya Azam FC na Simba unatarajiwa kupigwa Agosti 17 uwanja wa Taifa.
Mchezo huo ni wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 23 ambapo mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Mabingwa watetezi Simba na JKT Tanzania uwanja wa Taifa.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania 'TFF' Clifford Ndimbo amesema kuwa kiingilio kwenye mchezo huo kwa jukwaa la mzunguko ni 5,000 na Jukwaa la VIP B na C itakuwa 10,000.
Mchezo wa ngao ya Jamii huwakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu Bara ambao ni Simba pamoja na mabingwa wa Kombe la Shirikisho ambao ni Azam FC.
Nimesoma Gazeti Moja Maarufu La Michezo Leo Limesemema Ngao Ya Jamii Itipigiwa Samora Iringa Na Blog Hii Inasema Uwanja Wa Taifa Ukweli Ni Upi?
ReplyDeleteMzee Mkapa aliwahi kusema, kuna wakati waandishi wa habari wanatakiwa kurudi shule. Hii blog haina mhariri ama mhariri ana shida. Kila siku unaelezwa yaleyale. Ingekuwa darasani tungekuita kilaza. Msidhani kuandika ni taaluma, Bali unaandikaje kwa ajili ya nn ndio taaluma hutumika sasa
ReplyDeleteKwa mujibu wa TFF pambana limerudishwa kwa Mkapa na litachezwa Jumamosi July 2019 saa 1 usiku.
ReplyDeleteTFF wamesema wamebadili uwanja kwa sababu za kiufundi.
July 19
ReplyDelete