August 22, 2019




UONGOZI wa Lipuli umesema kuwa hesabu kubwa kwa msimu mpya ni kufanya vema tofauti na msimu uliopita.

Msimu uliopita Lipuli ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya sita ikiwa na pointi 49 baada ya kucheza michezo 38.

Itafungua pazia lake dhidi ya Mtibwa Sugar Agosti 24 uwanja wa Samora.

Ofisa Habari wa Lipuli FC, Festo Sanga amesema kuwa maandalizi yapo vema na wapo tayari kwa kuanza ligi.
.
"Tumefanya maandalizi mazuri na tupo tayari kwa ajili ya ushindani, kikubwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki na malengo yetu yapo wazi tunahitaji kumaliza tukiwa nafasi tano za juu,' amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic