August 11, 2019


PATRICK Aussems,raia wa Ubelgiji ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa matokeo waliyoyapata jana kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya UD Songo sio mabaya kwani bado wana nafasi ya kupata ushindi.

Simba jana ilicheza mchezo wa kwanza wa kimataifa kwenye hatua ya awali dhidi ya UD Songo, uwanja wa Beira nchini Msumbiji mpaka dakika 90 kukamilika ubao ulikuwa unasoma 0 kwa UD Songo na Simba pia.

"Tumefanya kitu kizuri kutoruhusu bao, juhudi kubwa za wachezaji wangu pamoja na juhudi za wapinzani zimeshindwa kuzaa matunda hivyo tunajiaanda kwa ajili ya mchezo wetu wa marudio.

"Mchezo wetu wa marudio Dar, tuna nafasi ya kufanya vizuri, mashabiki watupe sapoti tutapambana," amesema.

Simba itarudiana na UD Songo kati ya Agosti 23-25 jijini Dar, uwanja wa Taifa.

7 COMMENTS:

  1. nani ametoka taifa salama mbele ya simbaaaaaa?

    ReplyDelete
  2. Hakuna ndugu yangu. Mnyama hawakumuweza nyumbani kwao vipi wamuweze nyumbani kwake

    ReplyDelete
  3. Simba atashinda vizuri tu....tatizo liko kwa Yanga tu....hao wengine Azam na KMC wana nafasi nzuri pia kusonga mbele

    ReplyDelete
  4. Ud songo sio timu ya kubeza Simba wajipange waisibweteke. Ila tu kama benchi la ufundi la Simba litaendelea na pacha ya kagere na Boko hakutakuwa na mabadiliko yoyote yatakayoisaidia fowadline ya Simba kutopoteza nafasi za wazi za magoli. Sio siri na wala si uonevu bali Boko anatakiwa kubadilika. Anatakiwa kuwa makini zaidi ya alivyo sasa anaonekana kukosa kujiamini kila siku zikisonga mbele.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Boco anasumbuliwa na fatique kwani toka ligi iishe hajapumzika.....Ausems jana ameigharimu timu tacticaly....na anakariri......Boco+Mkude jana waliharibu chemistry ya timu.Hii ni kwa sababu walikuwa na taifa stars wakati wenzao wakiendelea na kambi south Africa for almost 3 weeks

      Delete
  5. Simba haitaweza kuifunga ud songo dar, safari yao imeishia hapa mwaka huu

    ReplyDelete
  6. Kocha awe makini na upangaji ndio maana wakati mwingine viongozi wanaingilia boko hakuwa anafanya lolote na walioingia hawakuleta mabadiriko yoyote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic