AZAM FC leo inashuka uwanjani kutupa karata yake ya kwanza mbele ya Fasil Kenema kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.
Azam FC iliyo chini ya Kocha Ettiene Ndayiragije ina kazi ya kutafuta atokeo ugenini kabla ya kurudaian na wapinzani wao Bongo uwanja wa Chamazi.
Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Chamazi.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga alisema kuwa
tayari kikosi kimeanza kuyazoea mazingira nchini Ethiopia hivy wana uhakika wa
kupata matokeo.
“Kocha Mkuu, Ndayiragije
ameandaa mbinu mpya za kutafuta ushindi hivyo kazi iakuwa kubwa na ngumu.
“Mashabiki
watupe sapoti kwani tunajua kwamba tuna kazi ngumu ugenini hasa ukizingatia
michuano hii ya kimataifa ni hatua ya mtoano tupo tayari,” amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment