August 25, 2019


Kama hatajwi sana lakini ni moja ya soka ndani ya miamba wa Msimbazi, Simba SC kutokana na mchango wake wa kuiwezesha timu hiyo kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Chama anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha leo kitakachocheza dhidi ya UD Songo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo.

Songo wakiwa kama wageni wa leo, walishindwa kuitumia bahati ya Uwanja wao wa nyumbani katika mechi ya kwanza kwa kwenda suluhu ya 0-0 na Simba.

Wakiwa ugenini leo wanaenda kukutana na mwamba huyu wa Lusaka aliyeng'ara zaidi msimu uliopita, kwa kuimaliza AS Vita pale kwa Mkapa akipokea pasi maridhawa kutoka kwa Haruna Niyonzima ambaye kwa sasa amesharejea kwao AS Kigali, Rwanda.

Chama amekuwa mzuri zaidi katika upikaji wa mipira haswa katika eneo la kiungo japo kuna wakati amekuwa akiamka vibaya lakini ndiye aliyeipa Simba mafanikio makubwa katika mashindano hayo msimu uliopita.

Uwepo wake leo unaweza pia kuwa chachu ya ushindi Simba tukiangalia rekodi zake kwenye msimu uliopita.

Ikumbukwe pia kiungo huyo alifunga bao maridhawa kabisa pale kwa Mkapa dhidi ya Nkana Red Devils katika ushindi wa 3-1, balo lililopatikana akipokea pasi maridhawa kutoka kwa Hassan Dilunga.

Chama anakipiga kwa mara ya kwanza Ligi ya Mabingwa msimu huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam akiwa na mastaa kama Sharaf Shibou, kiungo aliyekuja na makali ya aina yake msimu huu, kiungo ambaye anaweza kukimbia na mpira, kupiga chenga na hata vichwa, tena kwa hilo usipime.

Mbali na Shiboub, pia Simba ina wachezaji wengine kama Miraji Athuman, Gerson Fraga na wengine wapya waliosajiliwa.

Tusubiri tuone mechi itamalizika vipi, ni kuanzia saa 10 kamili jioni ya leo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic