ZESCO UNITED KUKUTANA NA YANGA KWA MKAPA
Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Green Mamba ya Eswatin umewafanya miamba hao wa Zambia kukutana na Yanga katika mechi ya raundi ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga watakipiga na timu hiyo inayonolewa na Kocha wake wa zamani, George Lwandamina aliyeondoka kimyakimya nchini baada ya kushindwa kulipwa stahiki zake.
Kuelekea mechi hiyo, endapo Yanga watafanikiwa kuiondoka Zesco wataingia hatua ya makundi ya ligi hiyo.
Na pia kama wataondolewa, watashuka mpaka Kombe la Shirikisho Afrika kwa ajili ya mechi ya mtoano ya kuelekea kufuzu makundi.
Yanga pia inakutana na Zesco kufuatia ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya Township Rollers ya Bostwana ilioupata jana.
0 COMMENTS:
Post a Comment