UONGOZI wa KMC leo unaanza rasmi mazoezi ya kuiwinda Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Agosti 27 uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwary Binde amesema kuwa kikosi kinaanza mazoezi leo uwanja wa Bora kujipanga na mchezo wao wa ligi.
"Tupo sawa na wachezaji wanatambua kuwa kazi inahamia kwenye ligi, tuna imani ya kupata matokeo kwani tupo tayari," amesema.
Mara ya mwisho walipokutana uwanja wa Uhuru, msimu uliopita, Azam na KMC zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment