ADAM Salamba mchezaji wa Simba dili lake la kujiunga na timu ya Polokwane FC ya Afrika Kusini limebuma na sasa anarejea Bongo kujiunga na kikosi cha Namungo FC.
Salamba ambaye alisajiliwa na Simba msimu wa 2018/19 akitokea Lipuli FC ameshindwa kwenda na kasi ya Simba na ametolewa kwa mkopo.
Awali Polokwane FC walikuwa wanahitaji huduma yake, habari zinaeleza kuwa hawajafika mwafaka na uongozi ambao umeamua kumpeleka Namungo
Salamba amesema kuwa msimu ujao ataitumikia timu hiyo yenye ngome yake Lindi.
Huyu salamba ni bure kabisa limbukeni kafika simba badala ya kutoboa zaidi lakini anazidi kujichimbia kaburi.Ukishindwa kupata namba Simba kutoka nje ya Tanzania nakwenda kufanikiwa ni nadra sana. Kwa Simba walivyo sasa wanamisingi ya kumuezesha mchezaji kwenda kufanya vizuri huko endako lakini kama alikuwa anafanya vizuri hapa Simba. Ushauri kwa wachezaji vijana pale simba hasa nawelenga Rashid Juma na Gadiel Michell ni kwamba uwezo wanao wa kufika mbali zaidi ya simba.Kuna wachezaji wenye umri wao tayari ni mastaa klabu kubwa kama Real Madrid nakadhalika.Moja wa shetani mkubwa kabisa katika maendeleo ya mwanadamu ni kukosa kujiamini.Ngedere ana kimo cha paka lakini anamvimbia mnyama kama Simba na Simba hufika mahala anaamini yakuwa huyu bwana mdogo anaweza kunizuru na mwishowe Simba huachana kabisa na ngedere nakumuacha na hamsini zake.Watanzania tuna maneno mengi kuliko kazi.Maneno mengi ni dalili tosha ya mtu aliekosa kujiamini.Mpira ni mazoezi. Mazoezi ya pumzi.Mazoezi ya nguvu. Mazoezi ya kula mlo sahihi ili kuujenga mwili kwa ajili ya kazi ngumu. Mazoezi ya kulala kwa wakati ili kuupumnzisha mwili na akili ili uwe na ufanisi wake bora. Mazoezi ya akili katika kuiga na kujifunza kwa wale waliofanikiwa.Mazoezi ya tabia kujiepusha na tabia mbovu kama vile ulevi na vitendo vyengine viovu kama uvutaji wa sigara na kujiepusha na kuambatana na watu watakaokutoa kunako malengo yako. Nakadhalika nakadhalika. Kwa jicho langu la haraka kama Rashid Juma atajiimarisha kunako utimamu wa mwili wake kutamuongezea uwezo wa kujiamini zaidi anapokuwa na mpira kitu ambacho kitampelekea kufanya maamuzi sahihi katika finishing zake iwe katika kutoa pasi au kufunga.Anatakiwa kujaza mguvu zaidi kunako kichwa chake kwa maana ya akili kuliko kunako miguu yake. Kuna vitu doga sana anahitaji ili aikamate namba pale simba kuelekea caf champion league ambayo naamini ni ticket kwa vijana wetu kupata timu za uhakika za kuwaendeleza zaidi kwa wale wenye malengo ya kufika mbali.
ReplyDelete