SIMBA KUILIPIA YANGA KIKAO NA WAANDISHI
Na George Mganga,
Dar es Salaam
Uongozi wa Simba kupitia Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema utalipia gharama za kikao na waandishi wa habari ambacho wamedhamiria kukifanya kitakachohusisha wasema wa klabu zote zinazoshiriki mashindano ya kimataifa.
Tanzania Bara inawakilishwa na timu nne kunako michuano ya kimataifa ambazo ni Simba SC pamoja na Yanga zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa huku Azam FC na KMC FC zikishiriki Kombe la Shirikisho Africa.
Katika kikao na waandishi wa habari juzi, Manara alisema kuwa watafanya kikao hicho kwa ajili ya kuungana pamoja kuonesha utaifa sababu wote wanaiwakilisha nchi.
Alieleza kuwa wao kama Simba watahusika kugharamikia kikao hicho kwa kuwa wana uwezo wa kufanya hivyo.
"Tumepanga kufanya kikao cha pamoja na wasemaji wa timu zote zinazoshiriki mashindano ya kimataifa.
"Lengo letu kubwa ni kuonesha kwanza utaifa kwa kuwa tunaiwakilisha nchi, hakuna sababu ya kutofautiana, lazima tupeane sapoti.
"Sisi kama Simba tutagharamikia kikao hicho, hilo halitakuwa na shida sisi kwetu kama mabingwa wa nchi," alisema Manara.
Huo ndio uzalendo na uungwana
ReplyDeleteHongera sana manara na huwo ndo uzalendo
ReplyDeleteHizo ni dharau sasa
ReplyDeleteManara sijakusoma vizuri! Try again.
ReplyDeletedharau kwani ameambiwa yanga hawana uwezo wa kulpia acha dharau ww ucyejtambua kkao umektaka ww sasa maneno hayo ya kejeli ya nn?
ReplyDeleteHawa jamaa wamekuwa watete Sana wanayo Ile inayoitwa inferiority complex wanahisi wao kama vile wanaonekana wa hali ya chini masikini na kuona wanadharauliwa na hata wakitajiwa kuzuri wao wanakiona kibaya
ReplyDeleteUhamasishaji wa Manara Ni wa hali ya juu wakusisimuwa na kutisha. Mungu kampa kipaje
ReplyDeleteNajua Yanga hawatakuja
ReplyDeleteHicho kikao Yanga wakikiudhuria watakuwa wamejidhalilisha kwani Manara siyo msemaji wao na pia si anayepanga ratiba yao. Hata hivyo Manara siyo msemaji wa Simba bali ni Mhamasishaji wa Simba hivyo amwombe msemaji wa Simba akutane na wa Yanga wapange jinsi ya kukutana na Yanga watakuwa tayari kulipia kikao hicho.
ReplyDeleteHicho kikao kinachotaka kupangwa wala hakikuja wakati mwafaka,kwanin wasingefanya kabla ya game za kwanza wakati Yanga yuko nyumbani?wanasubir wao mechi zao za nyumbani ndio waweke hamasa,hio wala haitokuwa msaada kwa yanga,maana ya kikao ni kuhamasisha pia washabiki kujitokez kwa wingi uwanjan na kushangilia timu zetu za tanzania,wakati timu moja kati ya hizo ipo ugenini,,
ReplyDeleteHaji is the big Brand.Elimisha vyura sports the way to support the gamez
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
DeleteAngekuwa mzalendo angefanya hilo wakati yanga inacheza hapa sio amesubiria simba inakuja kicheza home ndio anajinadi mzalendo.Wazo zuri ila atalifanya kwa maslahi ya timu Fulani.Kingefanyika wakati timu zote hazijaanza mechi za kimataifa
ReplyDelete