August 9, 2019


KUELEKEA kwenye michezo ya kimataifa ambayo inatarajia kuanza kesho kwa timu nne za Tanzania kupeperusha Bendera ya Kimataifa, Uongozi wa Simba umewazuia mashabiki wa Simba kuzomea wawakilishi wa Taifa.

Simba na Yanga zimekuwa na utamaduni wao hasa inapofika suala la kushangilia kimataifa ambapo imekuwa kawaida kwa timu moja kshabikia wapinzani jambo ambalo uongozi wa Simba umelikemea.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa: "Imetuchukua miongo kadhaa kama nchi kupata fursa ya kuwakilishwa na vilabu vinne kwenye mashindano ya CAF,
Na Simba ina mchango katika hili.


"Kama Taifa tunatakiwa tufanye vizuri zaidi kupitia wawakilishi wetu ili tuendelee kwa miaka ijayo kuwa na klabu nne katika CAF Competitions (michuano ya Caf).


"Najua ni ngumu kunielewa leo lakini nawaomba Wanasimba wote kesho msizomee Yanga, msilipe kisasi na wekeni maslahi mapana ya nchi, sisi ni waungwana na uungwana ni vitendo.

"Kama hujiwezi usiende Taifa na ikibidi kwenda na huwezi kuwashangilia bora ukae kimya.Najua walitukera msimu uliopita lakini tuiangalie nchi kwanza na pia tujue wao,Azam na KMC pamoja na sisi ndio tuna nafasi ya kuendelea kupewa nafasi nne tena msimu ujao.

"Naiangalia Tanzania kama nchi,utani na kuzodoana kwetu utatugharimu sote,kama kuwacheka tuwacheke baadae lakini kwa sasa interest (maslahi) ya Tanzania iwe moja," amesema.

11 COMMENTS:

  1. Leo umeongea kwa ustaarabu sana na unapaswa kuwa hivi kama msemaji wa Klabu kubwa nchin siyo yale makorokocho yako. Pia kumbuka Yanga hawakuwa na utamaduni wa kuizomea Simba ila Simba kupitia wewe mwenyewe Manara mkaanza kufanya hivyo mwaka 2016 wakat Yanga ikishiriki kimataifa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umezaliwa mwaka 2000 nini?... unajua neno Uzalendo umetushinda lilitokea mwaka gani?

      Delete
  2. kweli kabsa walvaa mpk jez za tp mazembe na haikuwa sawa tatzo la kupenda kuropokaropoka naona anaanza kubadlka anafuata nyayo za akn dsmas ten au jafar idi za kuongea maneno ya hekma (pamoja sana uzalendo kwanza) na mungu ataajalia tu wote tutashnda na tutafka mbali kla la kheri tanzania na tmu zote nne.

    ReplyDelete
  3. My country comes first Tanzania oyee

    ReplyDelete
  4. Utamaduni huu wa kijinga wa kuzomeana ulianza zamani sana sio 2016 kama mtoa maoni hapo juu anavyojaribu kutuaminisha.

    ReplyDelete
  5. Haswaaa hili litaendeleza mpira wetu kimataifa zaidi. Hata Yanga inatakiwa tuisapoti Simba hasa pindi watakapokuwa nyumbani kwenye mchezo wao wa pili. Kuzomeana tutisheke ligi ya ndani ili kuweka amsha amsha tu. Hongera sana Haji Sande Manara na uongozi wote wa Simba. Tunawaomba kesho mtufundishe jambo lingine zuri tuige kama hili la wiki jana.

    ReplyDelete
  6. Naamini ni jambo jema sana kusapotiana ili fursa ya timu nne kuendelea kushiriki mashindano haya makubwa isipotee

    ReplyDelete
  7. Kauli imekuja wa kati mbaya. Hats Simba wote waujaze uwanja kuwashangilia kwa Township rollers Yanga hachomoki. Kubeba gunia la misumari then inakuchoma mgongoni. Kila mmoja apambane na hali yake. Simba hatuhitaji support ya Yanga ili tushinde kimataifa.

    ReplyDelete
  8. Simba,nina maana ya mashabiki wa Simba wanaweza kabisa bila ya shaka yeyote kujizuia kuizomea Yanga lakini kwa mashabiki wa Yanga kitu hicho ni kigumu. Kumbuka Manara hii sio mara ya kwanza kuwaomba mashabiki kutoshabikia timu za kigeni zinapocheza na timu zetu.Alitoa hii rai siku zilizopita Wanayanga wakamtukana na kumzodoa na kuapa kwa kumwambia asiwapangie timu ya kushabikia. Wengine wakamwambia anaomba msaada wa mashabiki wa Yanga kwakuwa simba ndio inayoshiriki mashindano ya kimataifa. Mashabiki wa Yanga hawakuishia hapo tu bali wao walijiapiza hata iwe vipi wao hawawezi kuishabikia Simba kimataifa.Sasa kiukweli ni ubumbula wa hali ya juu kuishabikia timu ngeni zidi ya timu ya nyumbani yaani inaonesha kiasi gani watanzania tulivyokuwa watu wa hovyo. Inaonesha kiasi gani watanzania tunavyoweza kuuza utanzania wetu kwa wageni kwa bei ya bure kabisa kwa kisingizio cha ushabiki. Inaonesha jinsi gani watanzania tulivyo na chuki na husda na roho mbaya kutotaka kuona mtanzania mwenzetu akipiga hatua ya maendeleo na ndio maana hata watanzania wengi walitoka kwenda nje kutafuta maisha mara nyingi wameshindwa kupiga hatua kutokana na roho mbaya za kitanzania za kutokuungana mkono sisi kwa sisi wenyewe kwanza mgeni baadae. Watanzania tunatakiwa kubadilika hatuwezi kujificha kwenye kichaka cha ushabiki na kuhujumiana sisi kwa sisi kumbe hiyo tabia ya usaliti ndio maisha yetu. Tubadilike watanzania linapokuja suala la kitaifa kwa kuungana kuwa kitu kimoja.Tunajua usaliti kwa muafrika au kwa wa Africa wengi watanzania wakiwemo ni pandikizo ghasi la muda mrefu kutoka kwa wakoloni kuhakikisha wanaendelea kuitawala Africa na watu wake kifikra,kiuchumi,kielimu na hata kimichezo. Wazungu wana kitu hiki kinachosema Rule of the conquering is to divide them in order to rule them forever. Yaani mkakati wa kuendeleza utawala hasa kwa nchi za kiafrica na watu wake ni kuwatenganisha kutokuwa kitu kimoja hata katika mambo madogo ya kawaida ili waafrica waendelee kuwaabudu na kuwategemea wazungu milele na huko ndiko kutawaliwa hasa kwa mwafrica huku wakimsifia mtawala. Kwani kwa wafrica mpira si mpira mpaka tuangalie ligi za wazungu.Mwanamke hawi mrembo mpaka awe na ngozi nyeupe nakadhalika nakadhalika hivi vitu havijaingia kwenye ubongo wa muafrica kwa bahati mbaya au katika njia ya kawaida katika utashi wa mwafrica la hasha. Vitu hivi vya kumuona mzungu ndio Mungu ni mchezo mchafu wa wazungu iliosukwa kwa kutumia mikakati mikali zaidi kutoka kwa wataalam wao wa mambo ya siri na ni vigumu kwa mtanzania au mwafrica wa kawaida kujua nini kinaendelea katika maisha yao ya kila siku na kwanini vijana wa kiafrica kila kukicha wanafikiria kuikimbia Africa.Na utaona mwenyewe Africa ni kama vile bara lisilokuwa na mwenyewe kwani wazungu ndio waamuzi wa mambo ya Africa licha ya kuwa Africa ni bara la pili kwa ukubwa duniani kwa ukubwa wa Ardhi lakini ni bara namba moja duniani kwa rasili mali asilia. Wamerekani waliuwana kinyama katika vita vikali ya wenyewe kwa wenyewe kwa idadi ya watu wote wa unguja na pemba na chenji inabaki kwa ajili ya kutafuta umoja wa kitaifa.Mshikamano kwa wananchi katika jambo la kitaifa sio suala la hiari ni jambo la lazima.kwa hivyo watanzania tubadilike tupendane kwa maslahi ya Taifa .

    ReplyDelete
  9. Umeongea good brother. Simba tunaweza ila wenzetu hawawezi. Nakumbuka hawa jamaa mwaka jana hakuna mechi ambayo hawakuwashangilia wapinzania. Nkana ndo kabisaaaaaa.... Yanga wakawa ndo wenyeji wao na wakatenga jukwaa lao na kushare na mashabiki wa Nkana waliokuja nao. Na sio hiyo tu, ni mechi zoooote ambazo tulicheza nyumbani hawa wenzetu walitutenda vibaya kwa kuungana na wapinzani. Hadi Kocha wao akashiriki kwa namna moja au nyingine katika kutoa ushirikiano kwa AS VITA na TP MAZEMBE. Ila sisi hatuna tatizo nao, hatutawazomea, ila Mungu atawalipia hapa hapa chini ya jua.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic