August 9, 2019

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa ni lazima madai ya wachezaji wanaoidai timu hiyo yafanyiwe kazi kabla ya kurejeshwa ndani ya kikosi hicho.

Juma Abdul pamoja na Andrew Vincent 'Dante' hawajajiunga na timu kutokana na kudai stahiki zao huku habari zikieleza kuwa wamesimamishwa moja kwa moja ndani ya klabu hiyo.

Mwinyi Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ameongea na wachezaji hao pamoja na viongozi ili kufikia muafaka mzuri kabka yao kurejea kikosini.

"Juma Abdul na Dante, hawa wana kesi ya msingi na wanachokidai ni haki yao lazima walipwe, nimewaambia viongozi kwamba wafanye juu chini hawa wachezaji wapewe stahiki zao ili wajiunge na timu.

"Kuhusu Yoondani yeye anaruhusa maalumu hivyo timu ikirejea ataungana nayo kwani hajagoma.

"Taarifa zao ninanzo na ninatambua kwamba wana kitu cha msingi hivyo imani yangu ni kwamba muda si mrefu mambo yatakaa sawa na wataungana na wenzao kuendelea kupambana," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Sasa ikiwa hela ya kuwalipa Hakuna tutafanya nini

    ReplyDelete
  2. Hata msimu uliopita hawakuwa na mchango wowote, kama abdul alikuwa analipwa mill 6 halafu anaishia kuwekwa bench na boxer wa mill 2. Kwa beki ya sasa hata dante hana nafasi kwa maboko aliyotoa msimu uliopita sidhani kama ana jipya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama hana jipya jinsi vyenye unaona walipeni stahiki zao wakatafute maisha yao.kweli gongo wazi mnamatatizo walikuwa lulu kwenu Leo hakuna kitu duuh

      Delete
  3. Wanadai fedha za usajili za Msimu uliopita, kwanini waiendelee na kazi wakati wanashughulikiwa. Hata hivyo, mchango wao ni mdogo sana kwenye kikosi kwa sasa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic