ACHANA NA BILIONI ZA GSM, YANGA YAPATA NEEMA NYINGINE MWANZA
Uongozi wa Yanga umesema kuwa utawapatia wachezaji wake fedha ambazo zilikuwa kama motisha kuhakikisha wanaitoa timu ya Township Rollers ya Botswana.
Uongozi huo uliahidi kiasi cha shiligi milioni 50 ili kuwaondoa wapinzani wao hao, ambapo mpaka sasa hazijatolewa fedha hizo huku uongozi ukipanga kuwapatia pindi watakapokuwa kambini Mwanza.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa fedha walizoahidi baada ya kufanikiwa kuwatoa Rollers bado hazijatoka, lakini wapo kwenye michakato ya kuwapa ambapo alidai fedha hizo watapewa watakapokuwa wameweka kambi jijini Mwanza.
“Ni kweli tuliwaahidi wachezaji kiasi cha shilingi milioni 50 wakiitoa Township na hilo limefanikiwa, tutawapatia fedha hizo wakishaingia kambini jijini Mwanza,” alisema.
Yanga, keshokutwa Jumatano, itasafiri kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United kutoka Zambia, mchezo huo utafanyika wikiendi ya Septemba 14-15, mwaka huu jijini Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment