DEREVA AFARIKI AKIWA ANAWAENDESHA WATALII
Dereva wa kampuni ya Utalii ya Leopard Tours yenye makao makuu yake jijini Arusha aliyetambulika kwa jina la Livingston Masawe amefariki ghafla wilayani Ngorongoro akiwa anawaendesha watalii ndani ya gari lake.
Kifo cha mfanyakazi huyo kimeibua taharuki Leo jijini Arusha baada ya taarifa za awali kudai kwamba chanzo cha kifo chake kilitokana na kwikwi ya mfululizo ambayo ilipelekea mauti yake.
Hatahivyo, jambo ambalo limelalamikiwa na baadhi ya madereva wa magari ya kuendesha watalii ni kwamba endapo marehemu angepata msaada mapema angeweza kuwa hai kwa kuwa umechukua saa 16 mpaka kupata msaada katika eneo la Ngorongoro.
Madereva hao wamedai ni jambo la aibu katika sekta ya Utalii kushindwa kuwa na gari la wagonjwa wa haraka (ambulance) au helicopter ya kuokoa wagonjwa walioko porini.
Itakumbukwa ya kwamba sekta ya Utalii ni miongoni mwa sekta zinazoliingizia kipato kikubwa taifa ukiondoa sekta ya madini lakini cha ajabu huduma kama ambulance na helicopter zinakosekana.
Ni muda muafaka sasa kwa Waziri wa maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalah kuamka na kusikia Kilio hiki kwa kuwa huwezi kuzungumzia kuboresha sekta ya Utalii bila kuzungumzia madereva wa utalii tunajiuliza hivi ingekuwaje kama mtalii aliyekuwa ndani ya gari kashikwa kwikwi kama dereva je angepataje huduma?
0 COMMENTS:
Post a Comment