EXCLUSIVE, YANGA WAIGOMEA VODACOM
Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Makamu Mwenyekiti wake, Fredirci Mwakalebela, umesema hautaweza kuvaa jezi yenye nembo nyekundu ambayo ni ya wadhamini wa Ligi Kuu Bara, Vodacom.
Mwakalebela amefunguka kwa kusema kuwa hawataweza kuvaa jezi hizo kwani hawana utamaduni wa kuvaa rangi hiyo bali kijani na njano pamoja na nyeusi.
Ameeleza uwepo wa hali mbaya kiuchumi kwao usiwe sababu ya kuwafanya wageuke kanuni, taratibu na katiba ya klabu kwani ni jambo ambalo haliwezekani.
Makamu huyo amewaomba TFF kupitia Rais wake, Wallace Karia, wazungumze na Vodacom ili kubadili rangi ya nembo hiyo ndipo wanaweza kuvaa.








Kila kukicha malamiko
ReplyDeleteVodacom hawo yanga wasiwaumize vichwa vyenu achaneni nao hawo yanga kwani kuna timu ngapi? Muwadhamini hawohawo vilabu 19 ondoa kabisa hawo yanga
ReplyDeleteTatizo lako hujitambui wewe
ReplyDeleteKila timu ina haki,kwani wakati wanajadili mkataba wa udhamini yanga walihusishwa?yanga inanguvu sana ya wananchi.
ReplyDeleteNguvu ya mdomoni .Hata kuchanga madeni imekuwa stori.Eti nguvu ya wananchi ??Nguvu ya soda labda.
ReplyDeleteSasa mbona mapovu?so utuachie timu yetu tuamue
ReplyDeleteThis is ridiculous. Hata mimi bush lawyer nimegundua mh. anaongea pumba. Kwa hiyo kila timu isio na rangi nyekundu kwenye jezi yake ibadili rangi ya mdhamini? Acheni uboya. Tufanye kazi kiueledi basi. Khaaaah
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteTAIFA GAS......MAJI YA AFYA.......SPORTPESA.......AZAM CO.LTD....GSM TANZ,LTD......hao ni baadhi ya wadhamini waliojitokeza kuwekeza kwenye klabu ya Yanga. VodaCom imekuja kudhamini ligi ya Tanzania na si Timu. Yanga ina utamaduni wake kuanzia nje hadi ndani ya uwanja. Mfumo na utaratibu katika vilabu vyetu hivi viwili ulikuwepo kabla ya mimi na wewe kuwepo na hata hao Vodacom hawakuwepo. Umaskni usikufanye ukauza utu wako.
ReplyDeleteTFF itafute njia nzuri ya kuweka masuala yake kuanzia kwenye mifumo ya mikataba ya udhamini na uendeshaji wa ligi na sio kukurupuka kwa mawazo alikyokupa mkeo usiku. Hadi leo suala la TV right ni mali ya TFF na bodi yake na si mali ya vilabu. Yanga na Simba mgao wao wa TV right (haki ya matangazo) ni sawa na Ndanda na Mbao FC. Lazima TFF iendeshe vizuri mambo yake.
TFF imeshindwa kutengeneza mfumo wa kujipatia pesa na nina wasiwasi wa Marketing manager (Afisa Masoko)..si wabunifu. Wanashindwa kutengeneza hata Super Eight??? yaani zile timu nane za juu zile na ligi itakayosimamiwa na TFF ili watengeneze pesa wamekaa kuwaza kutoza faini zisizo na maana. Hakuna ubunifu kabisa
kwa hyo unasemaje wasidhamini kisa utamaduni et kwa kweli kazi ipo sana, kwa nchi yetu pekee hili nalisikia tu.
Delete