HAJI MANARA AOMBA KIPINDI AZAM ILI KUMALIZANA VIZURI NA MSEMAJI MPYA YANGA
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameamua kuomba kipindi Azam ili kuchuana na Mwanahabari mwenzake aliyeteuliwa siku kadhaa zilizopita, Hassan Bumbuli.
Bumbuli hivi karibuni alitangazwa na uongozi wa Yanga kuchukua nafasi ya Dismas Ten aliyekuwa Msemaji wa klabu hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara aliandika akiomba awekwe pamoja na Bumbuli ili wazungumzie mambo ya Professionalism.
Kauli hiyo ilikuja kufuatia Bumbuli kumsema Manara kuwa amekuwa ni mtu wa propaganda tofauti na kufanya kazi kwa ueledi.
Manara alionekana kuchukizwa na kauli ya Bumbuli ambayo imezua gumzo kubwa jana mpaka kupelekea Manara kuanza kumjibu kwenye mitandao ya kijamii.
Azam TV mpeni hicho kipindi anachotaka,ila akae akijua kuwa yanga wao wako busy na mashindano ya kimataifa kwa hiyo hawana muda wa kupoteza kwa malumbano yasiyo kuwa na faida kwa timu yao,na najua hio ni njia tu ya kuwatoa yanga kwenye mipango yao ya maandaliz ya mchezo wao na zesco,,
ReplyDelete