MENEJA wa timu ya Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa tabia ya mchezaji kushindwa kutoa pasi kwa mchezaji mwingine ni ngumu kuitolea maamuzi hasa ukizingatia kila mmoja anatimiza wajibu wake ndani ya uwanja.
Klopp amesema kuwa kitendo ambacho alikifanya nyota wake Mohamed Salah kwa kushindwa kutoa pasi kwa Sadio Mane kilikuwa nje ya uwezo wake kwani kuna wakati mwingine Salah alikuwa akishindwa kutoa pasi na alifunga mabao yaliyoipa ushindi timu.
"Kwa upande wa kusimamia maamuzi hasa ya kutoa pasi kwa mchezaji ambaye ana uwezo wa kushinda ni ngumu hasa ukiwa nje ya uwanja, kuna wakati Salah alishindwa kutoa pasi na alifunga japo mara nyingine amekuwa akikosa.
"Kwa sasa naona kila kitu kinakwenda sawa na nimemaliza matatizo yao yote, kitu kizuri ni kwamba Mane hakuzuia kuonyesha hisa zake, mchezo wa mpira ni tofauti na michezo mingine," amesema.
Agosti 31kwenye mchezo kati ya Liverpool na Burnley Salah alishindwa kutoa pasi kwa Mane ambaye alikasirika na kulaumu kitendo hicho licha ya timu yake kushinda kwa mabao 3-0 mchezo wa Ligi Kuu England.
0 COMMENTS:
Post a Comment