KASEJA ATISHIA AMANI BURUNDI
Kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinashuka uwanjani leo hii kupambana na Burundi katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa 2022 huko nchini Qatar.
Hata hivyo, kipa wa timu hiyo, Juma Kaseja ameliambia Championi Jumatano kuwa kutokana na maandalizi waliyoyafanya anaamini kabisa wataibuka na ushindi katika mechi hiyo.
Alisema licha ya soka la Burundi kutokuwa na tofauti kubwa na la hapa nchini lakini anaamini watafanya vizuri katika mchezo huo utakaowaweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi ya kutafuta tiketi ya kufuzu kwa fainali hizo.
“Maandalizi yalikuwa mazuri, wachezaji wote tupo salama, kilichobaki ni kucheza dakika
tisini kusaka ushindi.
“Mchezo utakuwa mgumu kwani zinakutana timu mbili ambazo tunafahamiana wachezaji kwa sababu wapo Warundi wanaocheza Tanzania, hakuna jinsi, tutapambana kuhakikisha tunashinda mchezo huu wa kwanza, kabla ya kumaliza kazi nyumbani,” alisema Kaseja.
0 COMMENTS:
Post a Comment