September 4, 2019


Na George Mganga

Mwenyekiti wa zamani Simba SC, Ismail Aden Rage, amesema kuwa mshambuliaji Mtanzania anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, anastahili kucheza Arsenal endapo akitua Ligi Kuu England.

Kauli ya Rage imekuja kufuatia siku kadhaa zilizopita kufanyika kwa droo ya makundi kwa timu zitakazocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu ambapo Genk anayoichezea Samatta kupangwa kundi E ambalo moja ya timu zilizopo ni Liverpool ya England.

Rage amefunguka akisema kitendo cha Genk kupangwa kundi moja na Liverpool kinazidi kumpa nafasi Samatta ya kuonesha zaidi alichonacho duniani huku akisema endapo akienda England anastahili kucheza Arsenal.

"Kwa namna Samatta anavyojituma uwanjani, bidii na nidhamu aliyonayo tangu nimempokea Simba wakati akitokea African Lyon, ni mchezaji ambaye anastahili kucheza Arsenal.

"Kupangwa kundi moja na timu kama Liverpool pia Napoli tena kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ni mafanikio makubwa sana ya soka kwa mchezaji, nasi kama watanzania tunajivunia katika hilo.

"Mimi naipenda Arsenal, na kama ingekuwa ni klabu yangu lazima ningempa namba pale acheze na anaweza kufanya vizuri kabisa".

Katika kundi hilo, mbali na Liverpool, timu zingine zilizopo ni Napoli ya Italy na Salzburg kutoka Austrian.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic