September 4, 2019


Kocha Mkuu wa KMC ambaye amewahi kuzinoa Simba, Coastal Union na Kagera Sugar, ameipa tahadhari mapema Yanga kabla ya kuwavaa Zesco United kwenye mchezo wa kimataifa.

Yanga itamenyana na Zesco Septemba 14, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kabla ya kurudiana nao Septemba 26, mwaka huu nchini Zambia ikiwa ni mwendelezo wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mayanja alisema kuwa mpira wa sasa umebadilika na siyo kama zamani, kazi kubwa kwa Yanga inapaswa kushinda mchezo wa kwanza.

“Wachezaji wakipata ushindi mchezo wa kwanza ule uwezo wa kupambana na akili inaongezeka, ila kama watapoteza ama kulazimisha sare kinachofuata ni presha kwenye mchezo wa marudio na inakuwa rahisi kupoteza.

“Kwenye michuano ya kimataifa mbinu kali na akili ndizo zinamaliza mchezo mapema kwa kuwa wao wanapeperusha bendera ya kimataifa basi wabadili namna ya kufikiria na kujifunza kwa walioshindwa, watapata hasira za kupambana,” alisema Mayanja.

2 COMMENTS:

  1. Vita dhidi ya Yanga si ndogo....sasa tusubiri reaction ya wapenzi wa soka wa timu ya wananchi ....vurugu yake si haba ....itajengengeka dhana kuwa sheria na kanuni ziliundwa zikiwa na kusudio kwa mlengwa wa adhabu....Kuongoza Soka kwa chuki si "afya" kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania....mapungufu ya kiutendaji na kiutawala yanapoainishwa na kusemwa inakuwa makosa....uhuru wa kukosoa na kutoa maoni ni uhuru wa kikatiba ambao kila mtu anao uhuru huu usikandamizwe kwa kutunga kanuni na sheria...ili kuzuia watu kukosoa mapungufu yanayotokea katika uendeshaji na usimamizi wa tasnia ya mchezo wa soka hapa Tanzania.

    USHAURI
    Yanga msitoke nje ya reli jiandaeni na Zesco mashabiki waujaze uwanja wa Taifa..ili muudhihirishie umma Yanga ni baba lao

    Ahsante

    ReplyDelete
  2. Na vita dhidi ya Simba si ndogo? Hivi wewe mwandishi usipoandika juu ya simba unapata msongo wa mawazo au mfadhaiko wa moyo? Kiswahili unajua sasa kwa nini unaandika hapo kocha Simba...kwenye kichwa cha habari halafu ndani kumbe ni kocha aliyewahi kuifundisha Simba, Kagera na Coastal..Kama akili yako imekomaa umgeandika Kocha aliyewahi kuifu disha Simba, Kagera na Coastal...Unaandika kama mke mwenza wa Simba.komaa kialili na kitaaluma

    Usifute tafadhali!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic