Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema hakuna ukweli wowote juu ya kupewa mechi tatu na mabosi wake ambazo akipoteza atafukuzwa kazi.
Zahera amekanusha taarifa hizo wakati akizungumza na kituo cha Radio EFM jana jioni alipoalikwa kutuoni hapo kwa ajili ya kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu timu yake.
Zahera ameeleza kuwa hajapewa mechi hizo na yanayoandikwa mitandaoni hayana ukweli wowote ule.
"Nani kanipa mechi tatu? Hakuna ukweli wowote kuhusiana na hilo.
"Kwani Barcelona hawajafungwa? Mimi nitaendelea kuwepo ndani ya Yanga, yanayoandikwa si ya kweli", alisema Zahera.
Vita dhidi ya Yanga si ndogo....sasa tusubiri reaction ya wapenzi wa soka wa timu ya wananchi ....vurugu yake si haba ....itajengengeka dhana kuwa sheria na kanuni ziliundwa zikiwa na kusudio kwa mlengwa wa adhabu....Kuongoza Soka kwa chuki si "afya" kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania....mapungufu ya kiutendaji na kiutawala yanapoainishwa na kusemwa inakuwa makosa....uhuru wa kukosoa na kutoa maoni ni uhuru wa kikatiba ambao kila mtu anao uhuru huu usikandamizwe kwa kutunga kanuni na sheria...ili kuzuia watu kukosoa mapungufu yanayotokea katika uendeshaji na usimamizi wa tasnia ya mchezo wa soka hapa Tanzania.
ReplyDeleteUSHAURI
Yanga msitoke nje ya reli jiandaeni na Zesco mashabiki waujaze uwanja wa Taifa..ili muudhihirishie umma Yanga ni baba lao
Ahsante
Shida unaipenda yanga kuliko mpira...hoja dhaifu sn
DeleteMadhali anaogopwa atavuruga kila kitu
ReplyDelete