LIVE: KAGERA SUGAR 0-3 SIMBA SC, MECHI YA LIGI KUU BARA
FULL TIME: KAGERA SUGAR 0-3 SIMBA SC
Dak ya 90, zimeongezwa dakika tano mpira kumalizika.
Dak ya 87, anaingia Wilker da Silva kuchukua nafasi ya Meddie Kagere
Dak ya 78, anapiga pale, goooooli, anaifungia Simba bao la tatu
Dak ya 77, Simba wanapata penati baada ya Miraji kufanyiwa madhambi eneo la hatari, Anapiga Kagere.
Dak ya 71, Ajibu anatoka nje baada ya kuumia, kuna uwezekano akaenda moja kwa moja ama akarejea. Yes, anatoka na Dilunga anachukua nafasi yake.
Dak ya 61, Miraji Athumani anaingia kuchukua nafasi ya Deo Kanda
Dak ya 60, Faulo kuelekezwa Simba, Awesu amefanyiwa madhambi.
Dak ya 59, Kagera Sugar wanaonekana kuamka wakipambana kusaka bao la kwanza.
Dak ya 57, Kona inapigwa kuelekezwa langoni mwa Simba, pigwa pale Manula anadaka na unamponyoka, Santos anaokoa. Ilikuwa nafasi kwa Kagera kufunga bao.
Dak ya 55, Mwaliyanzi na mpira katika eneo la hatari la Simba kushoto mwa uwanja, anapasiana na Luhende lakini wanakosa maelewano, Simba wanaokoa.
Dak ya 54, Fraga na Kanda wanashindwa kutumia vema nafasi eneo la hatari mwa Kagera, mpira unaokolewa.
Dak ya 51, Krosi ya Mohammed Hussein inashindwa kufanya vema kushoto mwa uwanja, inakwenda nje.
Dak ya 50, Peter Mwalyanzi anachukua nafasi ya Yusuf Mhilu upande wa Kagera Sugar.Dakika 45 za kipindi cha pili kimeanza kwa Kagera kufanya mabadiliko, ameingia Juma Nyosso akichukua nafasi ya Eric Kyaruzi.
MAPUMZIKO: KAGERA SUGAR 0-2 SIMBA SC
Dak 45 za kwanza zimemalizika, zinaongezwa mbili kuelekea mapumziko. Na mpira umesimama, kuna mchezaji wa Kagera amelala chini.
Dak ya 41, Dakika nne zimesalia kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Dak ya 35, Mohammeeeeed Hussein anaifungia Simba bao la pili baada ya kupasiana vizuri zaidi pale mbele.
Dak ya 29, Nafasi nyingine kwa Simba Kagereee, anapisha na mpira aliokuwa amedhamiria kuupiga kwa kichwa kufuatia krosi safi ya Tshabalala.
Dak ya 28, Faulo nyingine kuelekezwa Kagera, pembezoni kidogo mwa mduara wa kati mwa uwanja.
Dak ya 27, Faulo inapigwa kuelekezwa Simba, ni karibu na eneo la hatari. Anapiga Awesu, Simba wanaokoa.
Dak ya 25, Tayari Manula ameshaanza, imekuwa faulo, Santos ameicheza akimdhibiti Awesu.
Dak ya 24, David Luhende anapiga kichwa ambacho kinakwenda nje kidogo ya eneo la Simba na kuwa golikiki.
Dak ya 22, Faulo inapigwa kuelekezwa Simba baada ya mchezaji Kagera kufanya madhambi, imeshapigwa na Kagera nao wanafanyiwa madhambi, sasa ni kuelekea Simba.
Dak ya 21, Kagere tena anawakosa Kagera Sugar kwa mara ya pili, ilikuwa hatari.
Dak ya 20, Shiboub anafanya maajabu hapa, anawazunguka mabeki wa Kagera Sugar na kupiga shuti kali lakini inakuwa kona.
Dak ya 17, Kagera wanajituma kupanga mashambulizi kuanzia nyuma lakini kuipita ngome ya Simba imekuwa ngumu.
Dak ya 15, Simba wanaonekana kumiliki mpira zaidi ya wapinzani wao, anaunyakua Kagere, lakini inakuwa ni faulo.
Dak ya 14, Mohammed Hussein anakosa nafasi kwa kushindwa kuweka kambani mpira ambao kama angetulia lingekuwa bao la pili.
Dak ya 11, Golikiki nyingine, mpira unapigwa kuelekea Kagera, wanapanda Simba kulifukuzia lango la Kagera lakini mawasiliano yanakuwa si mazuri na Ajibu anakosa nafasi ya wazi.
Dak ya 10, Mpira unarushwa kuelekezwa Simba, ni baada ya kutolewa nje, umerushwa na wanautoa, sasa unaelekezwa Kagera.
Dak ya 09, Ni faulo inapigwa kuelekea Kagera, anapiga Fraga, Mbrazil huyu. Tayari kashapiga lakini unakosa matunda.
Dak ya 08, Yassin anajaribu kukontro mpira eneo la kati mwa uwanja lakini Kagera wanamzonga na kuondoka nao, bado kasi ya mchezo haijawa kubwa.
Dak ya 08, Zimbwe anamiliki mpira, anajaribu kumpasia Ajibu lakini wanaokoa, sasa unarushwa kuelekea Kagera.
Dak ya 07, Ni golikiki, mpira unaelekeza lango la Simba.
Dak ya 04, Gooooli, Meedie Kagere anaipatia Simba bao la kwanza baada ya kuapasiana vema katika eneo la hatari.
Dak ya 02, Kagera nao wanarusha baada ya Simba kutoa mpira nje.
Dak ya 01, Kapombe anarusha mpira kueleka langoni mwa Kagera, umetoka, anarusha tena.
Dakika 45 za kwanza zimeanza katika uwanja wa Kaitaba.
Fannya mchezo na Mnyama. Ni mwiko kushangilia Simba. Tunataka comments za Maxime kabla ya kuingia mitini
ReplyDelete