Ushahidi wa kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Simba, Evans Aveva na wenzake, unatarajiwa kutolewa uamuzi Septemba 17, mwaka huu kama wana kesi ya kujibu au laa hii ni baada ya upande wa serikali kufunga ushahidi, leo.
Kesi hiyo inawakabili aliyekuwa Rais wa Simba, Evans Aveva, makamu wake Godfrey Nyange na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope.
Katika kesi hiyo, mashahidi wapatao 10 wamefanikiwa kutoa ushahidi wao kwa nyakati tofauti mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar.
Hata hivyo, jana shahidi namba tisa na namba 10 walitoa ushahidi wao mbele ya mahakama katika kesi hiyo ambayo inaongozwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Shahidi namba tisa, E9955 Detective Sergeant (DT), Faustine Emmanuel Mashauri ambaye anatoka katika Maabara ya Uchuguzi wa Maandishi ya Polisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Shahidi huyo aliieleza mahamaka jinsi alivyopewa kazi ya kufanyia kazi hundi pamoja na fomu za maombi ya kuhamisha fedha pamoja na sahihi.
E9955 aliieleza mahakama kuwa Septemba 4, 2017 akiwa kwenye maabara ya uchunguzi alipokea bahasha iliyofungwa ikitokea kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa alifungua akakuta kuna vielelezo pamoja na barua ya maombi ya uchunguzi wa vielelezo.
Aliendelea kulieleza mahakama kuwa vielelezo hivyo ilikuwa ni pamoja na hundi ya CRDB Benki, fomu ya kuhamisha fedha kutoka CRDB Benki kwenda benki nyingine pamoja na sahihi na majina.
Shahidi aliiambia mahakama kuwa alianza uchunguzi wake na aligundua kuwa zile sahihi zilifanana kabisa na wahusika ambao ni Godfrey Nyange na Evans Aveva baada ya kubaini, aliandika ripoti na kuirudisha Takukuru, aliendele kuwa anaiomba mahakama kupokea vielelezo vile kama ushahidi.
Kwa upande wa shahidi namba 10, Ledson Gideon Kasulwa kutoka Kampuni ya WAFEM Tanzania Ltd ambaye anadili na mzigo kutoka nje kupitia Bandarini.
Katika ushahidi wake aliiambia mahakama kuwa Simba alikuwa ni mteja wake na alileta ombi la kutolewa nyasi zao bandia bandarini na ambaye alileta nyaraka za kutolea mzigo aliagizwa na Aveva.
Baada ya ushahidi huo, Hakimu Simba alisema kuwa kesi hiyo inatarajiwa kutolewa maamuzi na kufahamu kama washitaki wanakesi ya kujibu au laa kesi hiyo imeahirishwa mpaka Septemba, 17, mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment