Katika kuhakikisha kuwa wateja wake wanaendelea kupata burudani za kitaifa na kimataifa, Kampuni ya MultiChoice imetanzaza rasmi kuwa mashindano ya riadha ya dunia yanayoanza leo (27/09/2019) katika jiji la Doha nchini Qatar, yataonyeshwa mubashara katika king’amuzi cha DStv.
Mashindano hayo ya aina yake yanayojumuisha wanariadha kutoka kote duniani yatashirikisha mamia ya wanariadha ambapo kutoka Ranzania kutakuwa na wanariadha 4 ambao wote wanashiriki mbio ndefu yaani Marathon.
Wanaoshiriki kutoka Tanzania ni Alphonce Felix Simbu, Stephano Gwandu Huche, Augustino Paulo Sulle na Failuna Abdi Matanga ambao wanaondoka nchini wakiongozana na kocha maarufu wa riadha hapa nchini Andrew Samson Panga.
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso amesema kuwa DStv itaonyesha michuano hiyo mubashara kupitia SuperSport chanel namba 13.
“Kama kawaida yetu hatutaki wateja wetu na watanzania kwa jumla wakose burudani ya michuano mikubwa ya dunia kama hii, hivyo tumehakikisha kuwa watashuhudia mashindano haya kupitia DStv” alisema Jacquelina na kuongeza kuwa hii ni fursa ya watanzania kuwashuhudia wawakilishi wao wakipeperusha vyema bendera ya nchi katika mashindano makubwa ya riadha duniani.
Wakati Failuna atakimbia tarehe 27 Septemba ambayo ni siku ya ufunguzi, wakimbiaji wengine watatu watakimbia siku ya tarehe 5 Oktoba ambapo wote wanashirikimbio ndefu za kilomita 42.
Kushiriki kwa wakimbiaji hao nguli kunaleta matumaini ya Tanzania kufanya vizuri hasa ikizingatiwa kuwa ni wanariadha wazoefu na wameshawahi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Mumbai Marathon ambapo Simbu aliwahi kutwaa medali ya dhahabu
0 COMMENTS:
Post a Comment