Ni kama doa limeingia juu ya kumpatia mkataba Kaimu Kocha wa Taifa Stars, Mrundi, Etienne Ndayiragije baada ya kupoteza mchezo wa jana ambao ni wa kuwania kufuzu CHAN dhidi ya Sudan.
Ikiwa uwanja wake wa nyumbani, Stars iliambulia kichapo cha bao 1-0 likifungwa na Yassir Mozamili katika dakika ya 61 kipindi cha pili.
Kutokana na kupoteza mchezo huo, kwa namna moja ama nyingine inaweza ikawa imepunguza nguvu ya Ndayiragije kupewa mkataba kama ambavyo amekuwa akipigiwa upatu na baadhi ya wadau.
Nguvu ya kumpigia debe Ndayiragije ilikuja mara baada ya kufanikiwa kuiondoa Burundi katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kwa njia ya matuta.
Ushindi ulipelekea wadau wengi kusema ni vema akapewa mkataba ikiwemo mchezaji na straika wa zamani wa Yanga, Amis Tambwe anayekipiga katika klabu ya Fanja iliyopo Oman.
Licha ya kupoteza jana, Stars bado ina nafasi kwani bado itakuwa na kibarua cha marudiano dhidi ya Sudan ambapo mechi hiyo itachezwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment