Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa iliwakabidhi hundi ya malipo ya shilingi milioni 825,913,640 kwa washindi wawili ambao ni Kingsley Simon Pascal wa Biharamulo, Kagera na Magabe Matiku Marwa wa Mara wiki iliyopita.
Kubadili maisha
Akizungumza kwenye ofisi za makao makuu ya SportPesa Tanzania, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Ndugu Tarimba Abbas alisema kuwa lengo la kampuni ni kubadili maisha ya watanzania katika upande wa kiuchumi hivyo wanajivunia kufanya kwa vitendo jambo hilo.

Aliongeza kwa kusema kuwa mbali na washindi hao kunufaika na
fedha hizo lakini pia serikali imevuna kiasi kikubwa cha kodi cha zaidi ya
shilingi milioni 160 ambapo si kwamba zimechangiwa na kampuni tu bali kupitia
washindi hao serikali imepata faida.
Ndugu Tarimba alisisitiza watanzania kuendelea kushiriki kucheza
na SportPesa kwani hakuna anayejua ni lini atafikwa na bahati ya namna hiyo.
“Kwa kuwapata washindi wa kiasi hiki kikubwa cha fedha tuna imani
tutayabadilisha maisha yao na familia zao na hivyo sisi tunajivunia sana kwa
hilo,” alisema.
Aidha, Tarimba aliongeza kwa kusema kuwa “Sio tu kuwa washindi
hawa wameshinda bali pia wamechangia kiasi kikubwa cha kodi ya serikali cha
zaidi ya shilingi milioni 160 ambazo zitasaidi kufanya mambo mbalimbali ya
kijamii.”
Tusikate tamaa
Nao kwa upande wa washindi wa Jackpot hiyo ambao waliambatana na familia zao waliwashukuru SportPesa kwa zawadi hizo kubwa na kuwasisitiza watanzania wengine kuendelea kucheza kupitia kampuni hiyo ili waweze kuibuka kidedea.

“Mimi nimekuwa nikishiriki mara kwa mara na kabla ya hapo
nilikuwa nimebet kwenye mikeka isiyopungua 16 au 17. Baada ya kujaribu mara
zote hizo namshukuru Mungu nimefanikiwa na ninawaasa watanzania wenzangu tusiwe
tunakata tamaa,” alisema Kingsley aliyeambatana na mama yake aliyejitambulisha
kwa jina la Neema.
Yeye ni milionea
Naye Magabe alisema kuwa hadi sasa watu wake wa karibu wamekuwa wakimpigia simu na kumtumia jumbe fupi wakiwa hawaamini kilichotokea lakini akasisitiza kuwa ni kweli yeye ni milionea kwasasa.
Naye Magabe alisema kuwa hadi sasa watu wake wa karibu wamekuwa wakimpigia simu na kumtumia jumbe fupi wakiwa hawaamini kilichotokea lakini akasisitiza kuwa ni kweli yeye ni milionea kwasasa.
‘Ni kweli kabisa mimi ni mshindi wa Jackpot ya SportPesa, watu
wangu wakaribu wengine hawaamini hadi hivi sasa lakini kadri muda utakavyozidi
kwenda mbele wataamini kama kweli mimi ni mshindi,” alisema Magabe
aliyeongozana na mkewe Elizabeth Wambura.
Ufundi vs bahati
Katika mkutano huo Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba aliwaambia watanzania kuwa michezo ya kubashiri mara nyingi huwa ni ya kutumia akili na mara chache sana ndio huwa bahati.
Katika mkutano huo Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba aliwaambia watanzania kuwa michezo ya kubashiri mara nyingi huwa ni ya kutumia akili na mara chache sana ndio huwa bahati.
Alisema kuwa unatakiwa kutumia akili nyingi sana ili kuweza
kupanga “mikeka” yako vizuri na asilimia chache zitatokana na bahati.
“Mara nyingi watu huwa wanadhani kwamba hii ni michezo ya
kubahatisha, hapana, hii ni michezo ya kiufundi ambapo mchezaji anatakiwa
kutumia zaidi akili yake huku bahati ikichukuwa nafasi kwa asilimia chache
sana,” alisema.

0 COMMENTS:
Post a Comment