September 23, 2019


Ndege ndogo ya Shirika la Auric Air imeanguka leo Jumatatu asubuhi Septemba 23, 2019, katika uwanja mdogo wa ndege eneo Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.

Ajali hiyo imetokea saa 1:30 asubuhi ambapo ilikuwa ikiruka kutoka Serengeti kwenda Arusha baada ya kushusha watalii.

Katika ajali hiyo, rubani na abiria mmoja wamefariki dunia.

Kamishna Msaidizi mwandamizi wa shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete, amethibitisha kutokea ajali hiyo.

“Tutatoa taarifa zaidi baadaye kwani sasa kazi inayoendelea ni kuokoa vitu na kuhifadhi miili,” amesema.

Mashuhuda wamesema ndege hiyo iligonga choo cha zamani na kuanguka huku wakieleza kuwa rubani wa ndege hiyo anmayesadikiwa kufariki anajulikana kwa jina moja la Nelson.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic