ANDREW Simchimba mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) leo aeibuka shujaa kwa kuipperusha bendera ya Taifa kwenye michuano ya CECAFA inayofanyika nchini Uganda.
Ngorongoro Heroes imeanza vema michuano hiyo, ikishinda mbele ya Ethiopia kwa mabao 4-0,Simchimba aliyekuwa kwa mkopo Coastal Union akitokea Azam FC, akipiga mabao matatu 'hat-trick' na jingine likifungwa Kelvin John.
Tanzania imepangwa kundi B kwenye michuano ya mwaka 2019 ikiwa pamoja na Zanzibar, Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment