Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Septemba 2, 2019 ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020 iliyoanza rasmi Agosti 24, 2019 na kufanya uamuzi ufatao;
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ametozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi hiyo, kinyume na Kanuni ya 14(2m) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.
•Klabu ya Yanga imepewa Onyo Kali kwa kushindwa kuhakikisha Kocha wake Mwinyi Zahera anaongoza benchi la ufundi la timu yake akiwa katika mavazi nadhifu na ya heshima.
Adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Vita dhidi ya Yanga si ndogo....sasa tusubiri reaction ya wapenzi wa soka wa timu ya wananchi ....vurugu yake si haba ....itajengengeka dhana kuwa sheria na kanuni ziliundwa zikiwa na kusudio kwa mlengwa wa adhabu....Kuongoza Soka kwa chuki si "afya" kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania....Yanga msitoke nje ya reli jiandaeni na Zesco mashabiki waujaze uwanja wa Taifa
ReplyDeleteZahera alikuwa akihisi kuwa yeye yupo juu ya kanuni na yupo huru kufanya au kusema anachotaka yeye mwenyewe bila ya kuingiliwa na yeyote
ReplyDeleteVita dhidi ya Yanga si ndogo....sasa tusubiri reaction ya wapenzi wa soka wa timu ya wananchi ....vurugu yake si haba ....itajengengeka dhana kuwa sheria na kanuni ziliundwa zikiwa na kusudio kwa mlengwa wa adhabu....Kuongoza Soka kwa chuki si "afya" kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania....mapungufu ya kiutendaji na kiutawala yanapoainishwa na kusemwa inakuwa makosa....uhuru wa kukosoa na kutoa maoni ni uhuru wa kikatiba ambao kila mtu anao uhuru huu usikandamizwe kwa kutunga kanuni na sheria...ili kuzuia watu kukosoa mapungufu yanayotokea katika uendeshaji na usimamizi wa tasnia ya mchezo wa soka hapa Tanzania.
ReplyDeleteUSHAURI
Yanga msitoke nje ya reli jiandaeni na Zesco mashabiki waujaze uwanja wa Taifa..ili muudhihirishie umma Yanga ni baba lao
Ahsante
Angekuwa mzungu wasingemgusa Ila mswahili mwenzetu ndo hivyo tena. Mavazi nadhifu ndo yapi hayo?
ReplyDeleteHuyu AI tunamjua..ni punguwani.
ReplyDeleteVita dhidi ya Yanga si ndogo....sasa tusubiri reaction ya wapenzi wa soka wa timu ya wananchi ....vurugu yake si haba ....itajengeka dhana kuwa sheria na kanuni ziliundwa zikiwa na kusudio kwa mlengwa wa adhabu....Kuongoza Soka kwa chuki si "afya" kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania....mapungufu ya kiutendaji na kiutawala yanapoainishwa na kusemwa inakuwa makosa....uhuru wa kukosoa na kutoa maoni ni uhuru wa kikatiba ambao kila mtu anao uhuru huu usikandamizwe kwa kutunga kanuni na sheria...ili kuzuia watu kukosoa mapungufu yanayotokea katika uendeshaji na usimamizi wa tasnia ya mchezo wa soka hapa Tanzania.
DeleteUSHAURI
Yanga msitoke nje ya reli jiandaeni na Zesco mashabiki waujaze uwanja wa Taifa..ili muudhihirishie umma Yanga ni baba lao
Ahsante
Kama kweli mnapenda maendeleo ya soka letu shughulikieni pia changamoto zinazotolewa na makocha wa club zetu, wao ni wataalam wa soka, heshimuni taaluma zao. Kuna malalamiko mengine yanakuwa na mashiko. Ili tuwe na timu ya taifa iliyo bora tunahitaji kuwa na kanuni bora za kuliendesha soka letu. Adhabu sawa, lkn je kero za msingi ziendelee kupigiwa kelele kila kukicha, hamuoni umuhimu kuwa soka linapaswa kuongozwa kisayansi pia? Kanuni bila kutatua kero za msingi ni kazi bure!
ReplyDeleteSasa ikiwa kocha hiyo suruali aliyovaa siyo ya heshima je wale wachezaji pale uwanjani wengine hushusha bukta zao mpaka kwenye makalio je wale ndio heshima au hamna la kusema nyie tff?
ReplyDeleteBasi na hao wachezaji waingie uwanjani na suruali
ReplyDelete