September 3, 2019

Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Septemba 2, 2019 ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020 iliyoanza rasmi Agosti 24, 2019 na kufanya uamuzi ufuatao:

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefungiwa kuiongoza timu yake katika mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kutoa shutuma na kejeli kwa Bodi ya Ligi katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

14 COMMENTS:

  1. Mbona bado mechi ya kwanza tu fine.Ajitayarishe na fine mwaka huu sio mchezo

    ReplyDelete
  2. Tuna Fungia Fungia wameanza mapemaaa kampeni

    ReplyDelete
  3. Haki ya mama hii TFF balaa si mnasema ninyi mnawaiga watu wa Ulaya igeni na uvumilivu mnapoambiwa ukweli

    ReplyDelete
  4. Ulaya hakuna upumbavu wa kulaumu marefa au chama cha mpira FA ukifanya hivyo kifungo na faini inakuhusu.

    ReplyDelete
  5. Walimlea sana msimu uliopita. Sasa ajue hawezi kuleta shutuma za kijinga bila ushahidi. Safi sana Bodi ya ligi na kamati ya siku 3.

    ReplyDelete
  6. Vita dhidi ya Yanga si ndogo....sasa tusubiri reaction ya wapenzi wa soka wa timu ya wananchi ....vurugu yake si haba ....itajengengeka dhana kuwa sheria na kanuni ziliundwa zikiwa na kusudio kwa mlengwa wa adhabu....Kuongoza Soka kwa chuki si "afya" kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania....Yanga msitoke nje ya reli jiandaeni na Zesco mashabiki waujaze uwanja wa Taifa

    ReplyDelete
    Replies
    1. heeeheee labda mjaze vibanda umiza kwa shs mia mia.mliagiza mashabiki toka mikoani na wakaja kwa gari za kubeba mikaa siku yenu ya wananchi na uwanja hamkujaza.Bado sana

      Delete
  7. Vita ipi?Kanuni lazima zifuatwe.Kwanini mwandishi hukuandika kwamba Masau Bwire amepigwa faini shillingi 200000 kwa kuingia uwanja baada ya mpira kwisha.
    Mshika kibendera Janet Balama nae amefunga miezi 3 kwa kukataa goli halali la pili la Ruvu Shooting Stars .
    Hakuna njama wala nini!Mwaka jana alilelewa sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Vita dhidi ya Yanga si ndogo....sasa tusubiri reaction ya wapenzi wa soka wa timu ya wananchi ....vurugu yake si haba ....itajengeka dhana kuwa sheria na kanuni ziliundwa zikiwa na kusudio kwa mlengwa wa adhabu....Kuongoza Soka kwa chuki si "afya" kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania....mapungufu ya kiutendaji na kiutawala yanapoainishwa na kusemwa inakuwa makosa....uhuru wa kukosoa na kutoa maoni ni uhuru wa kikatiba ambao kila mtu anao uhuru huu usikandamizwe kwa kutunga kanuni na sheria...ili kuzuia watu kukosoa mapungufu yanayotokea katika uendeshaji na usimamizi wa tasnia ya mchezo wa soka hapa Tanzania.

      USHAURI
      Yanga msitoke nje ya reli jiandaeni na Zesco mashabiki waujaze uwanja wa Taifa..ili muudhihirishie umma Yanga ni baba lao

      Ahsante

      Delete
  8. Aliendelea na vituko vyake hata akafikiri anaogopwa na Hakuna kiongozi aliyethubutu kumuwasa Kwa kuogopwa na matokeo yake Ni kuwa mnaanza kula matunda aliyokupandieni. Keshapoteza heshima yake. Walishindwa kumkunja samaki angali mbichi

    ReplyDelete
  9. Vita dhidi ya Yanga si ndogo....sasa tusubiri reaction ya wapenzi wa soka wa timu ya wananchi ....vurugu yake si haba ....itajengengeka dhana kuwa sheria na kanuni ziliundwa zikiwa na kusudio kwa mlengwa wa adhabu....Kuongoza Soka kwa chuki si "afya" kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania....mapungufu ya kiutendaji na kiutawala yanapoainishwa na kusemwa inakuwa makosa....uhuru wa kukosoa na kutoa maoni ni uhuru wa kikatiba ambao kila mtu anao uhuru huu usikandamizwe kwa kutunga kanuni na sheria...ili kuzuia watu kukosoa mapungufu yanayotokea katika uendeshaji na usimamizi wa tasnia ya mchezo wa soka hapa Tanzania.

    USHAURI
    Yanga msitoke nje ya reli jiandaeni na Zesco mashabiki waujaze uwanja wa Taifa..ili muudhihirishie umma Yanga ni baba lao

    Ahsante

    ReplyDelete
  10. Safi sana, sheria lazima zifuatwe........

    ReplyDelete
    Replies
    1. Vita dhidi ya Yanga si ndogo....sasa tusubiri reaction ya wapenzi wa soka wa timu ya wananchi ....vurugu yake si haba ....itajengeka dhana kuwa sheria na kanuni ziliundwa zikiwa na kusudio kwa mlengwa wa adhabu....Kuongoza Soka kwa chuki si "afya" kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania....mapungufu ya kiutendaji na kiutawala yanapoainishwa na kusemwa inakuwa makosa....uhuru wa kukosoa na kutoa maoni ni uhuru wa kikatiba ambao kila mtu anao uhuru huu usikandamizwe kwa kutunga kanuni na sheria...ili kuzuia watu kukosoa mapungufu yanayotokea katika uendeshaji na usimamizi wa tasnia ya mchezo wa soka hapa Tanzania.

      USHAURI
      Yanga msitoke nje ya reli jiandaeni na Zesco mashabiki waujaze uwanja wa Taifa..ili muudhihirishie umma Yanga ni baba lao

      Ahsante

      Delete
  11. pili kwa utashi wangu sijawahi kumuona kocha anavaa pensi lakini si avae hata bukta basi ijulikanw ni mwanamichezo? kwa nn atuvalie vipensi hii ni dharau kwa et anaifundisha timu kubwa tusiseme tutasema mpaka kieleweke tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic