September 1, 2019


Inaelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba upo kwenye mipango ya kushusha straika wa maana katika dirisha dogo la usajili.

Maamuzi hayo yanakuja kutokana na safu ya ushambuliaji wa Simba kuonekana na mapengo kadhaa tangu kuondoka kwa Mganda, Emmanuel Okwi.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema uongozi unajipanga hivi sasa kuhakikisha anakuja straika wa maana atakayezidi kiwango cha Okwi kwa ajili ya kuongeza makali.

Straika huyo atakuwa ni wa kimataifa na bado haijajulika nchi atakayotokea maana bado haijawekwa wazi.

Inaelezwa lengo kubwa la kuhitaji straika mwingine ni namna Simba walivyokosa umakini katika mechi na UD Songo ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika ufungaji wa mabo.

5 COMMENTS:

  1. Hii blog ukiendelea na uhuni huu itakosa wasomaji. Striker huyu hapa alafu unasema haijulikani nchi anayotoka ndo uhuni wenyewe

    ReplyDelete
  2. Hawakuajua kabla kama okwi ni muhimu???

    ReplyDelete
  3. Hawakuajua kabla kama okwi ni muhimu???

    ReplyDelete
  4. Hawakuajua kabla kama okwi ni muhimu???

    ReplyDelete
  5. Safu ya ushambuliaji ni afadhali ila beki ni mbovu kuliko na kama mngeendelea na club bingwa ugenini ingekuwa hamsa + hamsa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic