September 4, 2019


TUNA kazi kubwa kwa Taifa siku ya leo kwa wachezaji wa timu ya Taifa kuanza kupeperusha bendera kwenye michuano ya Kombe la dunia ambapo kete ya kwanza inakuwa leo nchini Burundi kabla ya kurudiana nao kwenye ardhi ya Tanzania Septemba 8.

Ushindani kwenye michuano mikubwa siku zote huwa ni mkubwa kutokana na maandalizi ya timu zote kujipanga na kuhitaji kupata matokeo chanya bila kujali inacheza na timu gani.

Hii ndio kanuni ya soka kwa kila timu kuhitaji matokeo chanya bila kujali ukubwa ama udogo wa timu na ushindi umejificha kwenye maandalizi mazuri.

Mbali na maandalizi bado kuna jambo la muhimu ambalo linahitajika ni sapoti kutoka kwa mashabiki ambao wao morali yao inawafanya wachezaji wapambane bila kuchoka na bila kukata tamaa.

Hapo ndipo ambapo wengi hushangaa ni namna gani wachezaji hupata nguvu ni maajabu ya mpira kwamba kelele ambazo mashabiki wanazitoa ni aina nyingine ya nguvu ambayo huwaingia wachezaji wakati wa kutafuta matokeo na kutambua kwamba kuna watu wapo nyuma wanawatazama.

Jambo la msingi kwa sasa Taifa kuungana na kuipa sapoti timu ya Taifa ambayo kazi yake ya kwanza kwenye michuano hii mikubwa ni leo mbele ya Burundi ambao ni majirani zetu na ndugu zetu wa karibu.

Uwezekano kwa timu yetu ya Taifa kufanya vizuri upo vizuri kwani maandalizi yapo sawa na kila kitu kinakwenda kama ambavyo kimepangwa ni suala la muda kusubiri nani atakuwa nani.

Wachezaji wote kila mmoja anajua jukumu lake mbali na kuwa uwanjani ama kufika nchini Burundi wamekabidhiwa bendera ya Taifa hapo anatambua hayupo peke yake bali yupo na mashabiki wa Tanzania yote.

Kazi iwe moja tu kwa mashabiki ambao watakuwa nchini Burundi iwe kwa wingi wao ama uchache kwani kwenye mpira hakuna mashabiki wachache kila shabiki ana thamani yake ndani ya uwanja kwa kuwa anaipa sapoti timu yake.

Kila mmoja leo awe na kazi moja ya kuipa sapoti timu ya Tanzania kwa kuishangilia bila kuchoka kwa kuwa wachezaji wanakazi kubwa ya kupeperusha Bendera ya Taifa na mashabiki nao wanapaswa wapaze sauti yao kuipeperusha Bendera ya Taifa kwa kushangilia timu.

Sapoti ya mashabiki ni kubwa na ina umuhimu katika kutafuta matokeo na kingine ni dua kwa ajili ya wachezaji ambao wanaanza kuirusha kete yao ya kwanza wakiwa ugenini .

Baada ya hapo sasa mchezo wa leo ukiisha tuna kazi nyingine tena uwanja wa Taifa shughuli yetu inahama jumla kutoka Burundi mpaka Tanzania unadhani mashabiki hapo tunakosaje kujitokeza Taifa.

Nina imani kwamba kwa wingi na nguvu ya mashabiki ndani ya uwanja wa Taifa balaa la wachezaji wenu wakiwa ndani ya Taifa huwa halisahauliki kama ilivyokuwa kwenye michuano ya Afcon namna walivyopata matokeo mbele ya Uganda nguvu ya mashabiki ilichangia kwani Uganda wenyewe walisema walitishika na nguvu za mashabiki.

Kwa sasa ni muda wa kuiombea timu yetu ya Tanzania ifanye vema kwenye mchezo wake wa leo ambao ni muhimu kwa Taifa pamoja na wachezaji wenyewe kwani wanatazamwa na wengi duniani.

Jukumu la wachezaji leo linapaswa liegemee kwenye kutafuta matokeo kwani mpira wa sasa umebadilika hata ugenini inawezekana kupata matokeo na kusonga mbele kwenye hatua nyingine.

Kazi kubwa kwa wachezaji kufanya yale majukumu ambayo wamepewa kwani kila mmoja anakazi yake ndani ya uwanja kikubwa ni kwamba wanapaswa wasisahau kwamba wao ni timu moja na kila mmoja ana kazi ya kupeperusha Bendera ndani ya uwanja kwa kutafuta matokeo chanya.

Ni wakati wa kutafuta furaha ugenini ili kuja kuimalizia ndani ya uwanja wa Taifa wenye rekodi njema kwa timu ya Taifa kupenya kwenye michuano migumu ambayo imeshiriki kabla ya kufikiria kurudi nyumbani nilazima kufikiria kurudi na ushindi kwanza.

Kwenye mpira kila kitu kinawezekana kwa wachezaji kuamua kufanya kweli bila kuzembea kwa bidii isiyo ya kaaida wote watafanya vema na Taifa litakuwa na furaha kwa kupata matokeo chanya hakuna kingine zaidi ya ushindi.

Juhudi za wachezaji leo ni sehemu ya ushindi, maelekezo ya benchi la ufundi yakifuatwa na pia wachezaji kuongeza uwezo wao binafsi basi kitakachopatikana ni kikubwa na furaha itakuwa ndani ya Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic