September 4, 2019



UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa wameanza kupanga mikakati upya kwa ajili ya kurejea kwenye anga za kimataifa kwa hesabu kali ili wasiangukie pua kama msimu huu.

Simba msimu huu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imeboronga mwanzoni katika hatua ya awali tofauti na msimu uliopita ambapo walitinga mpaka hatua ya robo fainali jambo lililopelekea kuongezwa kwa idadi ya timu shiriki kutoka mbili mpaka nne kwa Tanzania.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa maumivu waliyoyapata ni sehemu ya darasa kwao jambo linalowapa hasira ya kufanya vema wakati ujao.

“Tumetolewa na michuano inaendelea hili kwetu ni pigo kubwa na kwa mashabiki wetu, hakuna namna ya kukata tamaa mashabiki wanapaswa waukubali ukweli nasi tunajipanga kwa ajili ya msimu ujao.

“Makosa yetu kwa msimu huu yametuponza tukaanguka ndivyo mpira ulivyo kilichobaki ni kuinuka na kuendelea na maisha imani yetu msimu ujao tutafanya vema zaidi ya hapa, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

2 COMMENTS:

  1. Mtatisha nani labda humu ndani ambamo mnabebwa na tayari harakati za kuwakwamisha wapinzani wenu wa ndani mmeisha anza tangia jana.

    ReplyDelete
  2. Peleka ujinga wako huko.Chura ndio kabebwa.Mngefungwa 2 mtungi .Mshika kibendera wenu nae kafungiwa miezi 3.Mmsheanza visingizio kwani mnakuja hamna ubavu.Zesco ndio mwisho wa safari.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic