September 6, 2019


Kufuatia Bodi ya Ligi Tanzania (TPBL) kumfungia mechi tatu Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera pamoja na kumpiga faini ya shilingi laki tano kutokana na makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting, uongozi wa klabu hiyo umeamua kutinga katika Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kuripoti madudu yanayofanyika kwenye ligi.

Bodi ya Ligi imemfungia mechi tatu Zahera kutokana na kosa la kuitolea maneno mabaya bodi hiyo ikiwa ni pamoja na kumpiga faini ya Sh 500,000 kutokana na kuvaa mavazi yasiyostahili katika mechi hiyo ya Ruvu hali ambayo uongozi wa klabu hiyo haukufurahishwa nao.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alinukuliwa akieleza juu ya mabadiliko ya baadhi ya kanuni za ligi likiwemo suala la benchi la ufundi kuwa katika mavazi rasmi ya pamoja ikiwemo kocha kuvaa mavazi nadhifu.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amefunguka kuwa, tayari wameshaitaarifu wizara husika juu ya madhaifu ambayo yanajitokeza ndani ya bodi ili kuweza kuchukua hatua.

“Bodi ilitakiwa imuite kwanza Zahera na kumueleza makosa yake, hawezi kuisema bodi kama hakuna jambo, busara inasema kama mtu anazungumzia jambo mwiteni mumsikilize, bodi siyo Mungu ni watu tu, kwa mfano timu inatoka Gaborone na kuwasili Jumatatu ikitokea kwenye mechi ngumu ya ubingwa wa Afrika, Jumanne kunakuwa hakuna mazoezi na Jumatano mechi, hivi kweli kocha asilisemee hilo!

“Unapomfungia mechi tatu kwa nini usimpe faini aendelee kuifundisha timu, tumeshaiambia wizara haya madhaifu na tunasubiri majibu, itafika mahali Wanayanga tutasema na tukisema tutamaanisha, utafika wakati nasema tutasema na tukiwa na jambo letu nina uhakika hakuna wa kutuzuia moto wetu sasa wakati unawadia,” alisema Mwakalebela.

5 COMMENTS:

  1. Huo ni utoto mwakalibela,timu inamangement management ilishindwa nini kumwambia koja baada ya kurudi kutoka gabarone juu ya Sheria hizo mpya,Ina maana mnamwacha Zahera afanye anavyotaka huku mkisubiri kutoa rawama kwenye uongozi wa tff acheni uchinga yanga ni timu Kama yimu nyingine shiriki katika ligi hamna uspecial wowote

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wapi umeona kuna sheria ya mavazi kwa kocha???taja nchi yenye sheria au kanuni. Umeona alivyovaa Ndairajige kwenye mechi ya Burundi Vs Tanzania??kuna vitu vingi vya maana kwenye mpira na si haya mambo madogo madogo. Sidhani kama Watanzania uwezo wetu wa kufikilia ndio umeishia hapo kwenye hivi vitu vya kitoto. Twende tuangalie ni jinsi gani ya kuboresha mfumo wetu wa ligi ili kuondoa manung'uniko kwa wengi. Na naamini huwezi kusema kama hujaguswa...likikufika nawe utaona

      Delete
    2. Wapi umeona kuna sheria ya mavazi kwa kocha???taja nchi yenye sheria au kanuni. Umeona alivyovaa Ndairajige kwenye mechi ya Burundi Vs Tanzania??kuna vitu vingi vya maana kwenye mpira na si haya mambo madogo madogo. Sidhani kama Watanzania uwezo wetu wa kufikilia ndio umeishia hapo kwenye hivi vitu vya kitoto. Twende tuangalie ni jinsi gani ya kuboresha mfumo wetu wa ligi ili kuondoa manung'uniko kwa wengi. Na naamini huwezi kusema kama hujaguswa...likikufika nawe utaona

      Delete
  2. Hamna uspecial wowote.Kama hamtaki kufuata kanuni anzisheni ligi yenu.Ujinga mtupu.Ingekuwa mashindano ya CAF mngegoma?

    ReplyDelete
  3. Hao yanga wanataka kusujudiwa na wakiamini kuwa wao sana nguvu kuliko timu yeyote hapa nchini.dawa yao ni kuwaondoa kwenye ligi haiwezekani wao kila kitu hawataki na wanaona wao wanaonewa.x

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic